Mwanaume awakimbia wadada na kuwaachia bili Bar.

Tarah

Senior Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
140
Reaction score
160
Jana nimecheka sana sana kwa sababu wadada walikimbiwa na kuachiwa bili baada ya kula na kunywa kama vile hawatakula tena.Walikuja na mwanaume aliyeonekana ana hela hawa wadada walikuwa watatu wanaonekana ni wanachuo wa chuo kimoja hapa tabora.
Wakaagiza mavinywaji machupa makubwa sijui yanaitwaje kila mtu moja moja yapo kama soda ya mirinda nyeusi.Jikoni wakaagiza kuku wawili na chipsy mayai kila mtu wakala zote kwa uroho hawajabakisha hata shingo waroho sana.
Huyo mkaka aliagiza tu maji makubwa basi.
Baada ya bili kupelekwa huyo mkaka akasema ngoja akatoe hela kwenye Atm kumbe akawa amekimbia moja kwa moja huku wadada walikuwa wanapiga stori wanagonga na mikono sijui walikuwa wanasema nini.Muda ulivyozid kwenda nahisi wakampigia simu haipatikani ikabidi waanze kuhaha wamekaaa hapo mpaka usiku saa 3 ndio kuna mdada mwingine akaja kulipa hela wakaondoka.Nikasema jaman pole yao tu wakome kudowea vya wanaume saivi wamekuwa wachoyo sana wabahili sana sana wanaume wamekuwa wachoyo .
 
safi kabisa, ni hivyo kuna wadada hivyo hivyo brother cjui aliwatoa wapi..wamefika pale wakaambiwa waagize, wakaagiza mishikaki mia300 na savana 3 tatu, tukaona fresh tu, mzigo ukaisha, wakaagiza kuku wa kienyeji wawili, ikabidi nimuage brother...akasema leo watalipa, ckutaka kujua ilikuwaje baada ya mimi kuondoka ila cha ajabu nilikoelekea nilimkuta brother ashafika na yuko anapiga maji yake taratiibu...nilipomuuliza vipi, akajibu tayari..
 
Na nahisi hii ndiyo trend siku hizi. Na sana inawakuta girls, not women.

A woman sure can take care of her own bills and those of her man and fellow friends if she chooses to.

Girls are dependent on a man. Na ili kuonekana they are dating someone who matters they tag along a bunch of their friends.

If you cannot afford to party unless a man is paying your bills then grab a bottle of wine, play some music and enjoy in the comfort of your rooms.
 
Mkuu, haya sasa ni mateso kabisaaaa.... Maana hii lugha, Dahhh....[emoji29] [emoji29]
 
Ukipenda starehe uwe na uwezo wa kuzimudu.


Hali ngumu jamani muonee huruma mifuko ya wenzenu
Tatizo tukimuita mmoja, nayeye ana alika rafiki zake hata wanne.
Sasa hapo walifika kwanza wanamtathmini mwanaume, wakiona ananukia kama bank, basi wanaanza kuagiza mijidude mikubwa mikubwa, na ikiwezekana wanaagiza hata mbuzi mzima.
 
Kupitia comment's zako nakuza sana uwezo wangu ktk kuielewa lugha ya waingereza hasa ktk kusoma na kuzungumza(bado kuandika)
 
Na wewe siku nyingine ukienda Bar fuata kilichokupeleka,usipende kuchunguza yasiyo kuhusu,yaani umeacha kilicho kupeleka mpaka ukaanza kuwahesabia walivyo agiza mpaka wanavyokula,na ukaona wamekula Kuku bila kubakisha hata shingo?!!

Au ni wewe ndiye uliyekimbiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…