Mwanaume hata life likipiga u-turn usikubali kukaa kwa mwanamke

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
2,682
Reaction score
6,638
Ushauri wangu kwa wanaume: hata maisha yakuchapa vipi, usikubali kukaa kwenye nyumba ya mwanamke wako
Hata kama anakupenda kwa dhati, ipo siku utakumbushwa kuwa si kwako
Jitahidi ujipange, hata kwa kidogo, ili ujenge heshima yako na nafasi yako kama mwanaume
Mwanaume anatakiwa kuwa kichwa cha familia, si mgeni ndani ya nyumba. Kukaa kwenye nyumba ya mwanamke kunaweza kuathiri maamuzi yako na kuondoa mamlaka yako taratib✍️
 
Huu ni ushauri unaotokana na mfumo dume. Mambo yamebadilika siku hizi sana na mwanaume usiposhirikiana na mkeo katika kuchuma maisha yatakupiga sana siku hizi. Nawafahamu werevu wengi ambao wapo vizuri mno kiuchumi kwasababu wanashirikiana vyema na wake zao.
 
Kila analokwambia mwanamke litafakari sana kwa kina kwasababu huwa nyuma yake kuna maslahi ameficha kwaajiri yake pekee yake tu bila wewe.

Anaweza kwambia tupate mtoto sasa,lugha anayotumia ni aidha tunachelewa, au wewe ni mwanaume ambaye napenda watoto wangu wamuite baba,ila in reality inaweza kuwa ni alishajikana kuwa mke wa mtu na yupo tayari kuwa single mother, anajiwekea retirement plan watoto ndio insurance plan yake, anataka kumtumia mtoto kama kidhibiti mwendo na silaha ili aweze kumcontrol Mwanaume, mojawapo au yote.

So ukiona mwanamke anakwambia twende tukaishi kwenye nyumba yangu,amini nakwambia kuna jambo lake amelipanga na halitakuwa zuri kwako mwanaume.
 
Waswahili wanasema Kenge mpaka zimtoke damu ndo usikivu unaanza
 
Kwann unatumia huu muda kucomment hapa,fanya jambo moja,nenda kaoe mwanamke ambaye ana mji wake,nenda ukaishi nae hapo na usihangaike kuwa na kwako.

Ndio utaelewa kwanini kwenye movies mwanaume akigombana na mkewe mke ana mtamkia mumewe na kumwambia "get out of my house".😂😂😂😂
 
Maisha hayana formula jombi, popote kambi.
Usitweze tu utu wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…