Superb2014
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 9,266
- 7,426
Poleni na majukumu ya kila siku wana JF!
Iko hivi kuna Mwanaume mmoja alikuwa na ndoa yake ya Kikristo, ikatokea Mama Mkwe akawa anaumwa Kijijini ikabidi Mke wake akamuugeze Mama yake huko Kijijini.
Baada ya Mke kuondoka kwenda kijijini Mwanaume alianzisha mahusiano mengine na Mwanamke anayeishi na wazazi wake. Mapenzi yakakolea Mwanaume akahamia kwa mwanake na vifaa vyote vya ndani. Baadaye Mke akarudi kutoka kijijini akakuta tayari Mume wake alishahamia kwa mchepuko na vitu vyote vilivyokuwa ndani, mke akaamua kuendelea na maisha yake hapo ndoa tayari imeshavunjika.
Miaka imekwenda Mchepuko na Wazazi wake hawataki kumuona yule Mwanaume nyumbani kwao wanataka aondoke, Mwanaume anadai hawezi kuondoka inabidi alipwe fidia ya muda wake aliopoteza anataka Mchepuko umlipie kodi ya Chumba ili akaanze maisha yake. Juzi vifaa vyote alivyohamia navyo kwa Mchepuko vimehifadhiwa Store Mwanaume kashafukuzwa tayari lakini bado analalamika anataka fidia.
Karibuni sana kwa majibu.