Mwanaume kumbuka we ni wa thamani

Barikiwa mkuu.
 
Wewe ni simp. Kutwa kuwaza ngono.
Unaweza kuwa na thamani hata bila kuwa na mwanamke.
Mwanaume wa thamani anafahamu kusudi lake. Yesu alikuwa wa thamani sana bila kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanawake, alikuwa na msimamo na hakuyumbishwa.
Yesu alikuwa na thamani sana sawa, lakini alizaliwa Kwa kupitia tumbo la mwanamke tena bila kujamihiana , kama mwanamke hana thamani Mungu angemleta Kwa njia nyingine na kwanini Mungu asingemtolea Kwa mwanaume
 
Yaani wanaume huwa wanajishusha wenyewe, mtu anamiaka zaida 40 lakini kila anachofanya anapeleka Kwa mama yake na dada zake badala ya kujadili na mkewe sasa hapo akimuona mbulula atalaumiwa kweli? Na unakuta hao kina dada hawajulikani ni vichaa au wagonjwa, sasa hapo mwanaume utakuta anamsinhizia mkewe!
 
Yesu alikuwa na thamani sana sawa, lakini alizaliwa Kwa kupitia tumbo la mwanamke tena bila kujamihiana , kama mwanamke hana thamani Mungu angemleta Kwa njia nyingine na kwanini Mungu asingemtolea Kwa mwanaume
Kumtumia mwanamke sio ishu, fikiria, Yule ambaye anaitwa Mwokozi na Wakristo, Mungu aliamua Yesu azaliwe akiwa na jinsia ya kiume na si ya kike. Ndo ujue Mungu anavyothamanisha uanaume maana Yesu hakuwa mwanamke. Mwanamke alitumika kusaidia kuzaliwa kwake kuwezekane.
 
Kuna mwanaume mwenye hekima na mwanaume mpumbavu ila maarifa ya mwanaume haishushi thamani yake, kwasababu anaweza akaoa mwanamke mwingine na akapendwa ila mwanamke wa umri wake akabaki kuwa single mom au mke mwenza.
 
Kinachonifurahisha ni kwamba siku hizi hata wanawake nao wameanza kuamka na kutambua thamani yao, wameshatoka kwenye zile propaganda walizokuwa wanalishwa bibi zetu hadi kuamini kwamba mwanamke si kitu kwenye hii dunia, tatizo linakuja pale wanawake nao wanapoamka na kujitambua mayowe na matusi yanakuwa mengi toka upande wa pili
 
Yesu alikuwa na thamani sana sawa, lakini alizaliwa Kwa kupitia tumbo la mwanamke tena bila kujamihiana , kama mwanamke hana thamani Mungu angemleta Kwa njia nyingine na kwanini Mungu asingemtolea Kwa mwanaume
Mkuu haya ni mambo ya rohoni zaidi, tukizama sana tutatoka nje ya mada. Emb tujikite ktk mada. Mtoa mada kila anachozungumza ktk huu uzi ni LULU.
 
Mkuu thread zingine kubali tu zikupite bila kutia neno.

Asante.
 
Mwanamke mwenye thamani ni bikra tu.
Wasio bikra hawana thamani yeyote hata kama ameolewa.
 
Mwanamke mwenye thamani ni bikra tu.
Wasio bikra hawana thamani yeyote hata kama ameolewa.
Hiyo ni kwa mujibu wa kanuni gani ya kiulimwengu, ambayo inaamua kwamba mwanaume yeyote tu ana thamani, ila mwanamke thamani yake ni hadi awe bikira
 
Hiyo ni kwa mujibu wa kanuni gani ya kiulimwengu, ambayo inaamua kwamba mwanaume yeyote tu ana thamani, ila mwanamke thamani yake ni hadi awe bikira
Ni kanuni ya kiasili.
Mwanamke anapotolewa ubikra, inaleta hali fulani ya kisaikolojia ya kuwa bega kwa bega na mwanaume aliyekutana naye kwa mara ya kwanza, na inakuwa vigumu kusaulika. Kama mwanaume huyo akimfanyia ukatili na wakaachana, inamuathiri kisaikolojia na hapo itakuwa vigumu kuunganika na mwanaume mwenye thamani, namaanisha mwanaume mwema. Kwasababu ya trauma za kimahusiano, bikra inabaki kuwa kitu cha thamani mno ambacho mwanamke amepewa bure.
 
Kwanza kabisa jifunze kutofautisha kati ya nature na social constructs, ulichokisema wewe siyo kanuni ya asili bali ni mtazamo wa jamii nyingi toka enzi na enzi kwamba binti kamwe hawezi kumsahau mwanaume aliyemtoa bikira, na mara nyingi mitazamo fulani ikishajengeka kwenye jamii husika ikadumu vizazi hadi vizazi basi hiyo mitazamo huanza kuchukuliwa kama ndio asili lakini kumbe ilitengenezwa na watu kama sisi tu

Mimi binafsi nimeshakutana na wanawake kadhaa ambao wanakiri kwamba walishawasahau wanaume waliowatoa bikira na wala hawana mapenzi nao kabisa, na hata hivyo hilo suala la kuchukulia bikira kwa uzito haliko kwenye jamii zote duniani labda kama hujatembeatembea kwenye nchi za watu, nimegundua hizo imani kwa asilimia kubwa zipo kwenye baadhi ya jamii za africa na asia na ndio maana nikakuambia uniambie ni kanuni gani ya kiulimwengu inayoamua kwamba thamani ya mwanamke iko kwenye bikira yake tu na si kitu kingine chochote

Sasa wewe unaniambia kuhusu mitazamo ya baadhi ya jamii kwani mitazamo ya jamii fulani ndio kanuni za asili, ili jambo liwe kanuni ya asili halitakiwi kuwa subjective bali linatakiwa kuwa objective kwa maana kwamba uwepo wake hautakiwi kutegemea mitazamo binafsi ya watu, yani watu wa jamii zote duniani wanatakiwa naturally wawe na utambuzi juu ya hiyo kanuni bila kuathiriwa na external factors kama gender stereotypes nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…