Mwanaume mashine; Pitia hapa uone mashine za kisasa kwenye kituo kipya cha TV cha Lemutuz

Mwanaume mashine; Pitia hapa uone mashine za kisasa kwenye kituo kipya cha TV cha Lemutuz

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
lem.jpg


Wakati yakiwa yamebakia masaa machache kabla ya macho na maskio ya mamilioni ya watanzania kuhamishiwa downtown Bongo kwa tukio kubwa namba mbili mwaka huu ,huku namba moja likiwa lile la usomaji wa ripoti ya mchanga.

Mmiliki wa kituo hicho kikubwa cha televisheni amewaonesha mashabiki wake mashine kadhaa alizonunua Marekani na Ulaya zikiwa katika majaribio ya mwisho mwisho.

Baadhi ya mashine za kisasa zilizobahatika kutambulishwa na Lemutuz ni mashine maalum za kuongelea(mics), vifaa vya kukalia (maarufu kama viti), kamera za kisasa kabisa zenye uwezo mkubwa, extension cables zenye urefu usioelezeka, acs pamoja na mashine nyingine ndogondogo kama vifaa vya kunywea chai na super coffee.

Lemutuz amedai ubunifu na kila kitu kwenye studio yake kunaenda kubadilisha jinsi watu wamezoea kupokea habari na uenda ikawa ni revolution itakayodumu kwa miaka 100 ijayo.

Pia Lemutuz ametumia muda huo kuwaomba vijana waliomaliza vyuo vikuu kuanza kutuma maombi ya ajira katika kampuni hiyo kuwa ya utangazaji
 
Back
Top Bottom