Mwanaume mashine; Pitia hapa uone mashine za kisasa kwenye kituo kipya cha TV cha Lemutuz

Mwanaume mashine; Pitia hapa uone mashine za kisasa kwenye kituo kipya cha TV cha Lemutuz

View attachment 572587 Wakati yakiwa yamebakia masaa machache kabla ya macho na maskio ya mamilioni ya watanzania kuhamishiwa downtown Bongo kwa tukio kubwa namba mbili mwaka huu ,huku namba moja likiwa lile la usomaji wa ripoti ya mchanga. Mmiliki wa kituo hicho kikubwa cha televisheni amewaonesha mashabiki wake mashine kadhaa alizonunua Marekani na Ulaya zikiwa katika majaribio ya mwisho mwisho.
Baadhi ya mashine za kisasa zilizobahatika kutambulishwa na Lemutuz ni mashine maalum za kuongelea(mics),vifaa vya kukalia (maarufu kama viti),kamera za kisasa kabisa zenye uwezo mkubwa,extension cables zenye urefu usioelezeka,acs pamoja na mashine nyingine ndogondogo kama vifaa vya kunywea chai na super coffee.
Lemutuz amedai ubunifu na kila kitu kwenye studio yake kunaenda kubadilisha jinsi watu wamezoea kupokea habari na uenda ikawa ni revolution itakayodumu kwa miaka 100 ijayo.
Pia Lemutuz ametumia muda huo kuwaomba vijana waliomaliza vyuo vikuu kuanza kutuma maombi ya ajira katika kampuni hiyo kuwa ya utangazaji
Du hayo makamera kamera na vifaa vya kunywea chai ndo vifaa vya kisasa? Te te te te te te kW kwel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haha Evelyn Salt njoo uone extension cables zenye urefu usioelezeka
hahahahahaha
Yani mimi nasema waibe twiga wetu lakini wasije wakamuiba Lemutuz....Kwangu ni mmoja wa viumbe vinavyo nipa furaha sana hakika kila nikimuona huwa nafurahi sana....hakika Lemutuz ni nyara ya taifa
Hila hapo kwenye extensio cable zenye urefu usio elezeeka na vifaa vya kunywea chai na coffee hakika nimecheka sana.....Msaga sumu ni mtu mbaya sana...
 
Watanzania tunajua kumkatisha mtu tamaa. Nyie mwenzenu kathubutu kufanya hiko kidogo. Wengine mnambeza hapa ila hamna hela hata ya kununua mic moja ya laki 5 nyambf zenu. Mwacheni huyo jamaa anapigana na life lake. Hata akiwa na chumba ka choo haiwahusu. Mbona mna akili ndogo kama ya liso

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahahahaha
Yani mimi nasema waibe twiga wetu lakini wasije wakamuiba Lemutuz....Kwangu ni mmoja wa viumbe vinavyo nipa furaha sana hakika kila nikimuona huwa nafurahi sana....hakika Lemutuz ni nyara ya taifa
Hila hapo kwenye extensio cable zenye urefu usio elezeeka na vifaa vya kunywea chai na coffee hakika nimecheka sana.....Msaga sumu ni mtu mbaya sana...
Sijui msaga sumu huwa anawaza nini jamani. Sasa akimuongelea le mutuz ndo huwa nachoka kabisa hahaha
 
Msaga Sumu ktk ubora wake. Hivi Shigongo hajui pa kupatia hela? Kamata Msaga Sumu weka GPL watu wagombanie mazageti yako brooo
Kweli kabisa hakika Jf kuna vipaji.....Msaga sumu anajua kusimulia na kuremba story wangepiga hela sana... aisee hii taarifa naisoma kila muda nacheka sana hasa nikiangalia mambo yaliyomo kwenye picha hahaha
 
Sijui msaga sumu huwa anawaza nini jamani. Sasa akimuongelea le mutuz ndo huwa nachoka kabisa hahaha
hahaha daa mimi nasoma hii habari mara kwa mara nacheka sana....jamaa anajua sana kupamba story na kusimulia...
jamaa ana kipaji sana sijui kama ana fahamu hili swala....nimecheka sana hii story...kifaa maalum cha kunywea chai hahaha
 
Back
Top Bottom