Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
Kuna Hii Mentality kwenye Jamii, kwamba Mwanaume Masikini ndio mwenye Mapenzi ya Dhati sanaaa, kwamba anapomtongoza mwanamke, Eti wewe Mwanamke unapaswa kumkubalia na kumpenda tu sababu ana Penzi la dhati .
Mwanaume Masikini akiachwa utasikia "Sawa umeniachia tu kisa Sina Hela, nitapata tuuu n k n.k "..lakini uhalisia anakua kaachwa Kwa sababu zake zingine ambazo Mwanamke kashindwa kuvumilia.
Wanaume Hawa tukiwa Kijiweni, ndio utasikia kauli zao halisi, ni wanaume Jeuri, ambao pia ni wenye Wanawake wengi wengi, Wana viburi, Waongo ongo sana na waigizaji, wanaoahidi wasitekeleze, n.k
Sasa Mwanaume kama huyu anakuja Kuachwa na Mwanamke wake Kwa sababu ya mambo mabaya anayomtendea.
Huyo anajiwahi "Demu kaniacha kisa Sina Hela, lakini Mimi nilikua nampendaaa sana, Sijui kama atapata mwanaume mwenye dhati kama Mimi" na blaa blaaah kibao.
Dada zangu, Msikubali kuingia kwenye huo Mtego, akiwa Masikini umempenda lkn katika Mahusiano umeona kapungua Kwa mambo yanayogusa Hisia zako mfano, anakupiga, anakugombeza, hakujali Kwa kidogo chake, ni kamtu ka Wanawake, Kila saa unakafuma, MUACHE MARA MOJA.
Dada zangu, Ikitokea Mwanaume amekupenda Kwa dhati na mwenye kipato, wee mpende pia as long as umeridhika Kihisia, anakupenda, anakufanya ujione Mwanamke mwenye Thamani ... ila naye ukiona anakutenda mabaya yanayogusa Hisia zako naye MUACHE TU.
Sasa hapa, Usiwe wa kuacha acha tu na kuchukua chukua tu, hapana. Jipe Muda, boresha Thaman yako, Mwanamke ukiwa Huru kiuchumi, aiseee mwanaume atakuabudu.
Hawa Wanaume Masikini wanaojifanya ndio Wana mapenzi ya Dhati, wengi wao wakishapata Vipato, ndo hubadilika, na kuwaumiza kiasi Cha kuwafanya msijione na thamani !!.
Na Mwanaume Masikini unapaswa kua Muwazi na Mkweli, Usiwe muongo na mjanja mjanja sana, siku ukijulikana, utaumbuka. Wewe kua wazi Kwa mwanamke, aamue kukupenda au Lah.
Na Pia anapoamua kukupenda, nawe kua mkweli basi kwake, sio anakukubalia, alafu unaendelea kua Muhuni, mateso yaan Masikini Jeuri. Mwanamke akija kukuacha , unaanza kulia "Kaniacha kisa Sina Hela "... Hautapata mwanaume kama Mimi"
Dada, Furahia sana Kwa sababu ni kweli yeye ni mwanaume aliyekero kwako na Sasa utapata Mwanaume anayekufaa Kwa sababu wewe wastahili kilichobora Kihisia na Amani na Maisha Kwa ujumla.
Akiwa Masikini, mwenye Dhati na dhahiri na kweli unaona anakupenda ,yes mnaweza inuana na kufika mbali lkn shariti awe mwanaume Mcha Mungu, Hawa Masikini Jeuri wasomcha Mungu, wengi wakishatoboa Maisha, Anakukataa!
Na Nyie Wanawake pia, Umepata Mwanaume ana kipato, kaamua kukupenda Kwa dhati, Tulizana basi, humpendi kua wazi kua bwana Sikuhitaji, Achaneni na Ujanja Ujanja wenu wa sitaki nataka, unakula pesa ya mtu weeeee alafu weee hutaki kuliwa au unaliwa na jamaa zako wengine.
Wewe hujampenda mtu, Tulizana, acha Njaa, tafuta Pesa zako. Hii itawasaidia sana kupunguza Mauaji yenu!.
Mwisho niseme.
Kua Masikini au Mwenye Kipato, sio kigezo cha kua na Mapenzi ya Dhati!