Mwanaume mbembeleze mwanamke baada ya ugomvi, mtatuua kwa stress

Mwanaume mbembeleze mwanamke baada ya ugomvi, mtatuua kwa stress

Kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend au mahusiano yoyote yale lazima kunakuwepo na kuhitilafiana kwa hapa na pale

Linapokuja suala la kugombana ya wawili hao kinachofuata ni kusuluhishana mambo yaishe mapenzi yaendelee

Kunapotokea ugomvi wa kimahusiano sio siri sisi wanawake huwa tunaumia sana,na huwa tunapenda mahusiano yazidi kuwepo hasa kama uliyenaye ni yule wa moyo wako

Katika hali hiyo tunategemea mwanaume amuonyeshe mpenzi wake pamoja na kugombana bado anampenda na anampenda sana

Hapa tunamtegemea mwanaume baada ya kugombana,baada ya SAA moja mwanaume atakuwa na jukumu la kuweka mahusiano sawa,kwa kumtumia text za hapa na pale,za kumbembeleza mwanamke hata kama mwanamke ndo alikuwa na makosa,haijalishi nani kaanzisha ugomvi ila mwanaume ana jukumu kubwa la kuweka mahusiano sawa


Kwa sasa hali imebadilika sana kwa hawa wanaume,mnagombana,mnamaliza hata siku mbili hakutumii text,wala kukupigia sim,na kama mwanamke ataendelea kupiga kimya,kinachofuata ni mwanaume kuanza kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazieleweki,mara aweke za mwanamke fulani,mara aweke za wanawake na status kibao,au akae online muda mrefu ambapo si kawaida yake

Unabaki unajiuliza ina maana mahusiano yameisha,mbona sielewi,mapicha picha ya nini tena

Ukweli ndo huu,tunapogombana na ukamaliza masaa 2 bila kutuma sms au kupiga sim hata kuulizia kitu fulani,yaani huwa tunaumia sana

Na kama tangu ugomvi yamepita masaa 5 hujatuma sms, huwa tunahisi kuchanganyikiwa,sms inaingia unadhani ni baby kumbe za watu wengine au mitandao maumivu huwa yanatuzidi

Nyie wanaume acheni kuwatesa wawapendao,hamjui tu tunavyoumia

Ndo maana muda mwingine unasema bora usiwe kwenye mahusiano

Tubembelezeni basi baada ya ugomvi,hata kama sisi ndo wakosaji au hata kama ni nyie wakosaji
Jiongeze
 
Back
Top Bottom