Mwanaume mzima unaimba "Sukari nampatia tena", kweli?

Mwanaume mzima unaimba "Sukari nampatia tena", kweli?

Airmanula

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
3,527
Reaction score
5,762
Kama mwenyekiti wa Chama cha Wanaume Wa Shoka Tanzania nasikitishwa sana na hali ya hivi sasa ya baadhi ya wanaojiita wanaume, unakuta mwanaume kabisa kafungulia radio na anacheza kabisa kwa kujitikisa anaimba "Sukari nampatia tena"....tena akiwa anasema hivyo nakuambia analegeza macho na kujilamba midomo...hapo kashika Ice cream anailamba lamba, suruali imechanika chanika ( wanasema fashion) huku kaishusha chini ya makalio..

Hawa ndio WAUME watarajiwa, jamani wanawake mnaolewaje na wanaume wa namna hii? Tena mwanaume anauimba wimbo huo beti zote kwa ustadi wa hali ya juu kabisa ..zaidi ukiwakuta wanabishania " kusutana" wao kwa wao kuhusu Nandy na Zuchu nani bora unaweza kushika kichwa kwa mshangao. Kama mwenyekiti nimesikitishwa na hii hali.

Sasa ndio mana wanawake wanatafutana wao kwa wao sasa mana wanaona wanaume wenyewe ndio sisi tunaimba "Sukari nampatia tena" , wafanyaje? Nasema msikate tamaa warembo, wanaume wa shoka tupo sema ni ngumu kutujua inabidi uingie chimbo haswa kutujua.

Nawapa pole wanaume wa dizaini hio niliyoisema, mnatia AIBU SANA.
 
Raha jipe mwenyewe bana ebu waacheni waimbe, kwani wakiimba ivo inabadilisha nini? Mashine inatoka au?
 
Wanaume wote wanao imba na kulegeza sauti zao ni MAKHANITHI.

Asili yetu sisi wanaume ni ukakamavu suala la kuimba ni khasa kwa Wanawake,kama ilivyo suala la sisi kuhudumia familia na kuitunza ni khasa kwetu sisi.
 
Raha jipe mwenyewe bana ebu waacheni waimbe, kwani wakiimba ivo inabadilisha nini? Mashine inatoka au?
Kwaio ni sawa wakitikisa makalio yao na kulegeza macho ndizo raha hizo wanajipa sio??
 
"....tena akiwa anasema hivyo nakuambia"

Hii kauli umeitoa ukiwa kwenye hali gani ndugu mwenyekiti?

Mwenyekiti isije ikawa umenyanyua vidole vitatu juu tu maana hilo neno 'NAKUAMBIA' limekaa kishangingi sana. Samahani lakini

Wakuu endeleeni kuudambua huu uzi wa ndg. Mwenyekiti [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom