Mwanaume na mwanamke ni sawa kama binadamu lakini asili yao haitaki wafanane katika baadhi ya haki, majukumu, wajibu na adhabu

Mwanaume na mwanamke ni sawa kama binadamu lakini asili yao haitaki wafanane katika baadhi ya haki, majukumu, wajibu na adhabu

Lamzettttt

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2020
Posts
1,218
Reaction score
3,481
Assalaam Alleykum.

hakuna ubishi wowote kuwa mwanaume na mwanamke ni sawa kama binadamu na haki zao za kifamilia zinapaswa kuwa sawa kithamani. Kwa sababu wao wote ni binadamu na hivyo wana haki sawa.

Nukta inayopaswa kuangaliwa hapa ni kuwa mwanaume na mwanamke, kwa sababu ya tofauti zao za kijinsia, wanatofautiana katika mambo mengi. Asili yao haitaki wafanane. Nafasi hii inataka wasifanane katika haki nyingi, majukumu, wajibu na adhabu.

Katika nchi za Magharibi jitihada inafanyika sasa kuzifanya haki na majukumu yao kufanana, na kupuuza tofauti zao za asili na za ndani. Hapa ndio kuna makosa katika mtazamo na mfumo wa Kimagharibi.

Nukta inayobishaniwa ni suala la kufanana kwa haki siyo usawa wa haki kati ya mwanamke na mwanaume. Usawa wa haki ni nembo tu ambayo imewekwa kwa makosa katika zawadi hii ya Kimagharibi.

Ni katika muongo uliopita ambapo kutokana na harakati za pupa, nchi za Kimagharibi wameanza kumpa haki zake za msingi, lakini bado hajaweza kupata haki zinazochukuana na maumbile yake na mahitaji yake kimwili na kiroho.

Kama mwanamke anataka haki na usawa na furaha katika familia lazima alitupilie mbali wazo la kufanana kwa haki. Hiyo ndio njia pekee ya kuimarisha uchangamfu kati ya mwanaume na mwanamke. Katika hali hiyo, sio tu kwamba mwanaume atazikubali haki za mwanamke, lakini pia atakuwa tayari kumpatia, na katika baadhi ya mambo atatoa haki nyingi zaidi tena bila kumdanganya.

Ni muhimu kwamba nafasi ya mwanamke iangaliwe upya na apewe haki lukuki ambazo na ambazo amekuwa akinyimwa katika kipindi chote cha historia.

Hata hivyo, haifai kuiga staili na mifumo ya Kimagharibi kibubusa, mifumo ambayo imesababisha madhara makubwa huko Magharibi kwenyewe. Tunachodai ni kuwa kutofanana kwa haki kati ya mwanaume na mwanamke, kwa mujibu wa mipaka ya maumbile na tofauti zao ndio kutenda haki zaidi.

Hukidhi mahitaji ya haki za asili vizuri zaidi, hutoa hakikisho kwa furaha ya familia na huisukuma jamii mbele katika njia ya maendeleo bora zaidi.

Inaweza kukumbukwa kuwa tunadai kuwa haki ya asili inataka kwamba, katika baadhi ya mambo, kuwe na kutokufanana kwa haki ya mwanaume na mwanamke. Kwa vile linahusiana na falfsafa ya haki, suala hili lina sura ya kifalsafa.

Ni kejeli kusema kuwa Azimio la Dunia la haki za binadamu ambalo linatoa hakikisho la mfanano haki kati ya mwanaume na mwanamke, imeidhinishwa na Bunge la nchi fulani, wanaume na wanawake wa nchi hiyo wanapaswa kuwa na haki zinazofanana.

Wa sallaam.
 
haitatokea kukawa na haki sawa, hii ni mbinu ya kuvuruga umoja wa familia
ni sawa na kusema katika serikali mihimili yote wawe na majukumu sawa au haki sawa, siyo rahisi
na hii inawaumiza weak part,
 
Usawa kati ya mwanamke na mwanaume ndio umefanya imekuwa ni rahisi kuona uchi wa mwanamke kuliko wa kondoo iwe mitandaoni au live, kama unabisha niambie uchi wa mwanamke wa Afghanistan [emoji1023] upoje?
 
Usawa kati ya mwanamke na mwanaume ndio umefanya imekuwa ni rahisi kuona uchi wa mwanamke kuliko wa kondoo iwe mitandaoni au live, kama unabisha niambie uchi wa mwanamke wa Afghanistan [emoji1023] upoje?
Kuna ukweli katika hilo.!
 
haitatokea kukawa na haki sawa, hii ni mbinu ya kuvuruga umoja wa familia
ni sawa na kusema katika serikali mihimili yote wawe na majukumu sawa au haki sawa, siyo rahisi
na hii inawaumiza weak part,
Weak part ni ipi hiyo ???
 
Kuna maneno mawili ambao ni ngumu kuyaelewa "equality" and "equity".

Katika jamii tunaweza kuwa na equality ila sio equity hapa Kuna mifano kadhaa ;

Tuchukulie katika kazi au makazini unaweza mwanamke na mwanaume wakawa na access ya kila kitu ofisini na haki nyingine za kisheria kama likizo sasa ile likizo ya mwaka (Annual leave) kwa wote ile tunasema "Equality"

Sasa panatokea ishu ya uzazi ndo hapo itabdi itumike "equity" kwamba mwanamke apewa miezi kadhaa (maternity leave) na mwanaume apewe wiki moja (peternity leave) kwa sababu Wana mahitaji maalumu ya likizo iyo kutokana hali halisi.

Jamii yenye kujielewa lazima iendane na equity ili kuleta usawa nikiwa na maana kila mtu apewe kipaumbele kutokana na nafasi yake iwe ,jinsia ,ulemavu hata umri maana binadamu tuko tofauti kabisa.
 
Hiv mmeona Ile picha Kwa manara Leo kale kajamaa kafupi kanashindwa kuases tundu ya kujisaidia haja ndogo?
 
Back
Top Bottom