Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Kama mwanaume, inakuwaje unakubali na kuamua kuwa watoto wako walelewe na mke wako pekee na si wewe pia kama baba katika familia?
Nadhani ni muhimu kuuliza, kwa nini mwanaume angeweza kuchukua maamuzi ya kumwacha mke wake peke yake kubeba jukumu la malezi ya watoto kwenye ulimwengu huu?
Katika jamii nyingi, familia ndo msingi mkuu wa jamii zote duniani, kupitia familia ndo tunapopata viongozi, kupitia familia ndo tunapata walimu, madaktari na wahandisi.
Na imekuwa kawaida kuchukulia familia kama muundo wa pamoja baina ya baba na mama, ambapo wawili hao wanasaidiana katika kulea na kuleta watoto duniani.
Ni wazi kwamba jukumu la mama ni muhimu sana, lakini je, jukumu la baba linapaswa kupuuzwa kiasi hiki? Kuna watu ambao wanaamini kuwa baba wanapaswa kuwa na jukumu kubwa zaidi katika malezi ya watoto, si tu kwa kutoa fedha na usaidizi mwingine, bali pia kwa kuwa na ushawishi katika kukuza tabia na maadili ya watoto wao haswa mchango wa mawazo.
Hii inaweza kuwa na maana tofauti kwa kila mtu, lakini ni nini kinachofanya mwanaume kuwa na mtazamo wa kumwacha mke wake pekee katika jukumu hili? Je, kuna changamoto maalum zinazowafanya baadhi ya wanaume kujiona kuwa si sehemu ya malezi ya watoto wao?
Je, ni mambo ya kijamii au tamaduni ambayo yanawazuia wanaume wengi kuchukua jukumu la malezi kwa namna inayofaa?
Mara kadhaa tumepata vijana wengi walioharibika kimaisha ukiwauliza kuhusu wazazi wa kiume, wataishi kusonya na kudai baba hakuwahi kuwa sehemu ya maisha. Kuna tabia walizo nazo vijana wengi mtaani zinatokana na kutokuwepo kwa baba ndani ya nyumba.
Kuna tabia ndani ya jamii zinaibuka kutoka kwa watu waliokosa father figure, na mbaya ni kuwa mwanaume unaweza kumsomesha mtoto wako na kumpa matunzo wakati akiwa kwa mama yake ila mchango wako wa kumkuza kimaadili ni mkubwa sana. Mama ana mchango wake tofauti kabsa na Baba kwenye makuzi ya mtoto.
Kwa mwanaume ni sababu zipi zinakufanya ushindwe kabsa kuwa sehemu ya maisha ya mtoto wako? Na je, kuna umuhimu gani kwa baba kuwa sehemu ya malezi ya mtoto katika familia? Je ni maadili na tabia za mwanamke? Je ni tabia yako binafsi?