Mwanaume ukichepuka, mke au mpenzi akijua unajiweka hatarini

Mwanaume ukichepuka, mke au mpenzi akijua unajiweka hatarini

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
6,559
Reaction score
12,518
Hizi siku mbili tatu naona kidogo niwaletee mada za mahusiano tujadili sisi watu wazima.

Suala la kuchepuka kwa kawaida ni uhalifu ndiposa wanaofanya hivyo hutakiwa kufanya kwa kificho (sichochei bali nataka nitoe tahadhari kwa tafsiri yangu ya maisha niliyoshuhudia na kuona au kuhisi)

Matokeo hutokana ma mwanamke uliye naye na hapa nitajaribu kuweka katika makundi kadhaa:

1. Wapo wanawake wanaolipa kisasi kwa kuchepuka na wao, bahati mbaya ni kuwa wao hufanya kwa hasira bila kujali afya zao, sasa akikutana na mtu mwenye maambukizi halafu akarudi kwako tayari nawe unapata madhara. Rejea uzi wa kimasihara

2. Wapo wanawake wanaokutega uanze wewe ili wapate sababu ya kufanya na wao. Kawaida mwanamke ni mtu mwenye hofu kufanya makosa lakini akiona wewe umeanza anapata ujasiri, sio ajabu kusika mwanamke anakwambia hapendi mtu ambaye hachepuki sio kwamba yeye ni mwema bali naye anatafuta apate na yeye sababu ili asijisikie hatia atakapofanya na yeye. Mwanamke wa aina hii akiona hakamati nyendo zako mbaya, atachukia sana na anaweza kukwambia wazi wazi tahadhari ni ile ile mwanamke hajui kujilinda kulinda afya yake.

3. Wapo wanawake wanyonge ambao hawawezi kufanya lolote lakini atakusubiri na wewe siku uwe mnyonge apate nafasi ya kulipa kisasi. Mfano umeugua au umezeeka, wazee wengi waliowaumiza wake zao enzi za ujana hukumbana na mtihani sana wa kukataliwa au umeugua. Hii nimewahi kuiona sehemu kadha wa kadha.

4. Wapo wanawake wanaojibu papo kwa hapo kama vile kutumia silaha na kadhalika kama ni mfuatiliaji wa vyombo vya habari sio ajabu kusikia mwanaume amekatwa viungo vya siri na kadhalika. Mwanaume kuwa makini.

5. Wapo wanawake wanaopoteza hisia za mapenzi moja kwa moja na wewe, unakuta mnaishi lakini mwenza wako ameshapoteza hisia na wewe moja kwa moja na kama ni mjanja, lazima uta notice mabadiliko.

Wazoefu wa mahusiano watakuja kuongeza nyama kwenye huu uzi. Wewe rejea kusoma title tena 🤣
 
Kiukweli nikiwa na mahusiano sioni sababu ya kutafuta mahusiano mengine
Haikuagi rahisi hivo mkuu.
Sisi wanaume tuna tatizo la kukinai vitu.
Unaeza kuta mwanaume ana mke mrembo Sana nyumbani ila anachepuka na vitu vya ajabu ajabu huko nje.

Sisi wanaume hata tungekuwa na uwezo wa kujiumbia wanawake tunaowataka baada ya Muda fulani tutawachoka tu na kwenda kutafuta wengine huko nje.

Mfalme Daudi alikuwa anakosa mwanamke gani mpaka aamue kuchepuka na mke wa Uriah🤔
 
Haikuagi rahisi hivo mkuu.
Sisi wanaume tuna tatizo la kukinai vitu.
Unaeza kuta mwanaume ana mke mrembo Sana nyumbani ila anachepuka na vitu vya ajabu ajabu huko nje.

Sisi wanaume hata tungekuwa na uwezo wa kujiumbia wanawake tunaowataka baada ya Muda fulani tutawachoka tu na kwenda kutafuta wengine huko nje.

Mfalme Daudi alikuwa anakosa mwanamke gani mpaka aamue kuchepuka na mke wa Uriah🤔
Tatizo lenu na sio langu ,sijawahi kuwa kwenye mahusiano ni kachepuka na sita fanya hivyo .
 
Back
Top Bottom