Mwanaume ukiondoka kwenye familia inabidi pengo lionekane

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Wanaume tujitahidi sana sana kuwapenda wake, wapenzi wetu tunaoishi nao,

Busu(kiss) ni siraha tosha ya kuimalisha mahusiano, Asubuhi ukiamka mbusu mkeo, mpenzi wako kwenye paji la uso, shavuni na tumboni, jioni pia ukirejea kazini fanya hivyo hivyo na kumtakia neno "Nakupenda sana mke wangu" ata kama mkiwa mmegombana usisite kufanya hivyo ni faraja tosha.

Ni jambo dogo lakini ni kubwa sana kwenye mapenzi, Mwanamke mwingine anaweza kuchukulia jambo dogo kwa vile uko nae na unalifanya kila siku, Lakini ukiondoka safari ata ya siku mbili tu lazima alione pengo lako na kukumisi.

Wanaume tuonyeshe upendo kwa wake na familia zetu ata kama hatuna pesa, tuache chuki, hasira zisitawale mioyo yetu.

Upendo, upendo ndio nguzo kuu kwenye mahusiano yeyote.

Tujaribu kuficha sana hasira zetu ata pale tunapouziwa.


Cc Zero IQ

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…