Engager
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 1,522
- 3,255
Pengine wewe ni mwajiriwa ama umejiajiri. Unauwezo kifedha. Umemzuia mkeo kufanya kazi kwa sababu wewe unamtimizia haja zake zote kifedha. Unahudumia familia, na yeye as an individual unamhudumia. Pengine zaidi ya hata angefanya hiyo kazi. Kazi kwa maana ya shughuli yoyote inayoweza kumfanya yeye apate pesa yake. Iwe ya kuajiriwa ama kujiajiri.
Kunawengine wana biashara kubwa tu. Lakini hawawashirikishi wake zao. Kwamba mke anapaswa akae nyumbani alee watoto. Basi mke anakuwa ni wa kupokea tuu.
Nakushauri, hata kama unauwezo wa kuhudumia familia na mkeo kwa kila kitu, yaani kwamba mkeo hata akitaka leo ukajenge kwao huo uwezo unao na hutetereki, mwache tuu mama huyo nae aparangane.
Sio kwamba uache kumhudumia, endeleza huduma ila mwache aparangane, wakati mwingine kama unamuona ni mzito, msaidie awe mparanganaji japo kidogo, kwa maana hatuijui kesho.
Hivi kwamfano, wewe si ndo kichwa cha familia? Si unamhudumia mkeo, hutaki aparangane, yeye awe ni mpokeaji tuu. Vipi kama ikitokea umetangulia mbele za haki ukamwacha na hao wanao?! Do you know how helpless will she be?! Atawalea vipi hao machalii na wewe ulimzoesha kupokea tu? Ulisha wahi kufikiria ataanzia wapi?!
Sometimes hisia za mapenzi kwenye ndoa tuziweke kando. Tuache wake zetu waparangane hata kama tunauwezo wa kuwahudumia kwa kila kitu. Ni kwa manufaa ya kizazi chako.
Ni makosa makubwa kumzuia mke kufanya kazi.