Mwanaume unaemkataza mkeo kufanya kazi unafanya makosa makubwa

Halafu maisha saingine ni kama bahari yanakupwa na kujaa,

Siku Mwanaume hela ikikata akapata mtihani mtakula nini?

Ada za Shule za watoto mtalipia nini?
 
Wanaotaka mke awe goli keeper ni wanaume wenye akili finyu.

Wenye upeo huwa wanataka mke mzalishaji mali.

Wealth maximization sio mchezo mchezo.

Angalia Bill gate mkewe kama alikuwa maamuma goli keeper,

Angalia wake wa matajiri wote ni wazalishaji mali.
 
Mwanaume kwa kuwa Leo unavijisenti unazani uhakika wa kuwa navyo kesho upo pia?

Yanaweza kujitokeza mambo ukajikuta huna kazi, hivyo vijisenti vyako vikakata, utashika
Wapi Kwa mfano?

Mkeo akifanya kazi hata kama atakuwa mbinafsi wa hela yake lakini uhakika wa kula nyumbani utakuwepo,

Ada za watoto wenu atalipa labda awe na Roho mbaya kupita kiasi na mwenda wazimu ndipo shone kulipia wanae ada na kutoa hela ya kula maana hao wapo kwenye jamii.

Hata kama mke anapokea kodi ya Nyumba ananunua nguo nzuri ashindane na wenzie watoto kuwalipia Ada hataki anasema wakasome Shule za serikali ambazo nyingine hazieleweki perfomance yake.
 
Halafu maisha saingine ni kama bahari yanakupwa na kujaa,

Siku Mwanaume hela ikikata akapata mtihani mtakula nini?

Ada za Shule za watoto mtalipia nini?
Matokeo ya watoto ambao hawakusoma na matokeo ya watoto waliosoma kwa ada ya mama yao kwa baba zao hayana tofauti. Inaweza kuwa hujanielewa. Yaani ni hivi. Msaada wa watoto kwa baba ambao walisoma kwa ada ya mama hawana tofauti na ambao hawakusoma kabisa. Wenye mtazamo mkubwa watanielewa
 



Samahani Kwani kuna mahala nimeku-quote kwenye uzi huu?

Maana mimi nimechangia kutokana Na mada iliyopo!.

Nikajua labda wewe ndiye Mleta mada nimeona sio,

Sasa rejea iko wapi tulipoingiliana mimi na wewe mpaka unasema huenda sijakuelewa?

Halafu ulichoandika hapo sijui walosoma na walosomeshwa kwa hela ya mama sio Sawa sijakupata vizuri.
 
Sijaandika chochote huko nyuma. Kusema sijui kama umenielewa nilikuwa naongelea hapohapo kwenye hiyo reply yangu hapohapo. Nilimaanisha kwamba endapo kama mwanaume ataanguka kiuchumi moja kati ya matokeo mabaya ni kukosa elimu bora kwa watoto. Katika hoja yako moja kati ya manufaa ambayo atayapata mwanaume aliyepoteza uchumi wake ila mke wake anafanya kazi ni kusomeshwa kwa watoto wake kwa pesa za huyo mke wake.
Sasa kwa upande wa hitima ya furaha ya mwanaume kwa upande wake binafsi ni kuwa. Hakutokuwa na tofauti kati ya watoto ambao angepoteza uchumi na akashindwa kuwasomesha na mke wake haingizi chochote na yule aliyeanguka kiuchumi kisha watoto wake wakasomeshwa na mke wake kwa vile anafanya kazi. Hapa naongelea hitima ya mwanaume ye kama yeye
 



Ahaaa okey,
Ni maoni yako sikatai,

Lakini Kwani watoto wakisomeshwa na mama yao (mke wa jamaa) wakijakufanikiwa kwenye maisha watashindwa kumsaidia baba yao sababu walisomeshwa na mama yao pekee ?

Watakuwa na wazimu hao watoto si bure,

Hata kama mama yao atakuwa jeuri kujitapa kuwasomesha.

Halafu kina mama wasichojua kuwajaza watoto chuki wawachukie bana zao ni kuwapunguzia watoto hao Baraka za maisha.

Mama Kama unampenda mwanao hakikisha uhusiano wake na Baba yake unakuwa mzuri wakati wote.

Acheni upumbavu wenu,

Chuki zenu na waume zenu mnazipeleka kwa watoto wachukie bana zao, kwa kufanya hivyo mnawakwamisha watoto.
 
Mzazi siku zote usizae mtoto/ usilee au kutunza mtoto ukitegemea ukubwani atakukumbuka.

Tenda wema uende zako.

Mwanaume ategemei shukrani kutoka kwa watoto wake.
 
Ndo maana nikasema kuwa. Ni heli mwanaume aoe tu goalkeeper kwa kuwa hata hao watoto wakisomeshwa na mama yao baada ya anguko la uchumi watakuwa wamejazwa chuki tu kwa baba yao kitu ambacho baba yao hatonufaika nacho. Yaani kwa upande wake kama vile hawakusoma tu
 
Mzazi siku zote usizae mtoto/ usilee au kutunza mtoto ukitegemea ukubwani atakukumbuka.

Tenda wema uende zako.

Mwanaume ategemei shukrani kutoka kwa watoto wake.
Ndo maana tunasema nibora uoe mama wa nyumbani ili furaha yako uianze mapema. Ukijichanganya utakoswa furaha kotekote.
 



Lakini wapo watoto wachache hata wakijazwa chuki na mama zao badae hutafakari na kujirekebisha na kuanza kuwajali Baba zao.
 
Kama kipato kinatosheleza mwanamke hakuumbwa afanye kazi akae tu aletewe
 
Mi wangu ana pambana anapitilza.Anaeza enda shamba kulima mwezi mara ana kiduka kila siku anarudi home sa tatu usiku.
Bado ana vikundi vikao vikoba kila weekend.Lakini chakushangaza naona ana madeni mengi na hata sioni juhudi zake zinaishia wapi.
 
hiii kitu ni kosa kubwa mnooo kuna jamaa alimzuia mkewe kufanya kazi mkewe akaacha mambo ya kujishughulisha sasa jamaa ameachishwa kazi sahivi anajilaumu muda woote kwamba daaa ningejuaga nisingemuachisha angekua ananipiga kampani katika ipidi hikiii akamalizia na neno dadekiiii sijui ndio alimaanisha nini vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…