Mwanaume unawezaje kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili?

Mwanaume unawezaje kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili?

Kuna jamaa mmoja bonge flani hivi. Akienda ukweni anavaa taulo anaenda bafuni(bafu lipo nje uani)
Yupo comfortable anaona sawa. Binafsi huwa nashangaa
Sasa afanyejeee? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa sisi tuliooa WACHAGA,

Suala la kulala ukweni ni MARUFUKU! Yaani SAHAU!

Kwanza binti akishaolewa, YEYE mwenyewe haruhusiwi kulala kwao, sembuse wewe??

Mimi alifariki baba mkwe, nililala lodge wiki nzima. Kila siku naenda msibani asubuhi, usiku narudi lodge kulala.
Na mkeo ulikua unalala nae Lodge? Si umesema hatakiwi kulala kwao?
 
Kwa sisi tuliooa WACHAGA,

Suala la kulala ukweni ni MARUFUKU! Yaani SAHAU!

Kwanza binti akishaolewa, YEYE mwenyewe haruhusiwi kulala kwao, sembuse wewe??

Mimi alifariki baba mkwe, nililala lodge wiki nzima. Kila siku naenda msibani asubuhi, usiku narudi lodge kulala.
Hizi ndo mila sasa!! mila za kudumisha ndoa na kujenga uanaume asilia
 
Hilo neno la mwisho linaharibu utamu wa maudhui uliyotoa hapo juu yaani hapo umeonesha ww ni mwakilishi wa hao wanaokaa ukweni.

Back to the point kwakweli binafsi ukweni labda uwe ni msiba mzito ndo unaweza kuniweka siku3 kinyume cha hapo ni siku mbili au moja nasepa tena nitarudi huko baada ya muda mrefu kupita kama hakuna shida yoyote
Alitakiwa aseme nawasilisha
 
Mimi sijui kama ni ubaguzi au ni nini lakini utaratibu wao ndio uko hivyo. Mwanamke akishaolewa haruhusiwi kurudi nyumbani na kulala. Ataenda kusalimia tu asubuhi na kuondoka jioni kurudi kwa mumewe.

Na hii haijalishi hata kama mwanamke ameolewa nyumba ya 3 kutoka kwao, hawezi kwenda nyumbani kulala.

Binafsi niliona kama ni utaratibu mzuri
Hizi ndo mila originali, mila asilia
Siyo mila za kulea upuuzi, mwanamke ukimkoromea tu kaishakimbila kwao, na anapokelewa kabisa

Ukimzaba kofi ukoo wote unakusanyika, mpaka polisi unapelekwa
 
Kumbe huwa mnaishi kabisa….
Mimi ni siku mija tu…. Nampeleka wife… kesho yake nasepa.
Mimi sijawahi kulala kabisa, yaani nikikaa zaidi ya masaa 3 sijui nimepatwa na nini tena huwa sina mazoea na watu wa ukweni kwangu.
 
Sipendi kukaa ukweni, sipendi kukaa kwetu, sipendi kukaa kwa watu wala kwa mtu......
Nikienda kwetu sitaki izidi siku tatu.

Napenda na nna amani kukaa kwangu.
 
Siku 2 mkuu, Tena hizo siku zenyewe hushindi ndani, unajifanya kuna ishu unafatilia, siku ya tatu mapema!!
 
Back
Top Bottom