Naamini asilimia kubwa tunapenda kuonekana wa heshima tukiwa na wake zetu japo kuna maeneo lazima mke ajiachie sio manguo marefu kila sehemu. Mfano mnaenda ufukweni hakuna haja ya kuvaa manguo marefu na kingine usafiri gani unatumia huwezi toka na mkeo kavaa kimini alafu mnagombania daladala huo ni mtihani mwingine. Unenda dinner na wife avae manguo ya kanisani huo ni uongo. Kiufupi ni kwamba kila sehemu ina mavazi yake na mazingira yenu yatawafanya mjiachie au msijiachie. Mfano mm naweza safiri na wife from dar to klm kavaa bukta lakini hatuwezi safiri umbali huo huo tukiwa kwenye bus akavaa bukta au nguo nyepesi kulingana na mazingira.