Mwanaume wangu analewa kupindukia. Nifanyeje aweze kuacha?

Mwanaume wangu analewa kupindukia. Nifanyeje aweze kuacha?

Joined
Jun 5, 2024
Posts
2
Reaction score
5
Naomba ushauri.

Nina mwanaume wangu lakini ana tabia ya ulevi uliokithiri yani kulewa mpaka asubuhi na huendelea siku inayofuata mfululizo.

Kila wakati anaomba msamaha kubadilika hali ni ile ile. Kwa wazoefu unahisi anaweza kubadika au kwenye Ndoa vitendo vitazidi. Nimevumilia yapata miaka miwili now lakini bado tabia ipo.
 
kwa kweli swala la pombe ni swala gumu sana,

kwanza anatumia pombe gani?? ni beer au hizi kali za kwenye plastiki za siku hizi???

je anaweza kufanya kazi zake? kama ni beer tu anakunywa basi huyo bado hana matatizo sana ila kama ameshaingia kwenye hizi za kisasa za akina kisungura basi hapo anahitaji sala na maomnbi ya kutosha
 
Ulevi wake una athiri kwa kiasi gani shughuli zake au familia? kama hazina athari jitahidi asubuh unapoamka mtengenezee supu nzito na siku ameshinda nyumbani mtengenezee chakula kizuri ili akalewe vizuri.

Ila kama zina athari kwa familia na akzi zake mtafutie dawa inaitwa kilavoi
 
Pole Sana kwa changamoto hiyo,ila la kuacha Ni yeye aamue tu mwenyewe,indelea kumuombea
Mimi niliamua kuacha kabisa pombe mwenyewe. Sikuambiwa na mtu, na wala nilikuwa sinywi sana.

Sijanywa pombe yoyote tangu ninywe glasi moja ya Champagne kusheherekea kuingia mwaka 2024, January 1.

Uamuzi huu, kwa kiasi kikubwa, ni wa mtu mwenyewe.

Wengine wanaweza kusaidia tu.
 
Ni kweli kabsa bro,uamuzi upo mikononi mwa mme wa mtoa mada
 
Back
Top Bottom