Mwanaume wangu analewa kupindukia. Nifanyeje aweze kuacha?

Mwanaume wangu analewa kupindukia. Nifanyeje aweze kuacha?

Naomba ushauri.

Nina mwanaume wangu lakini ana tabia ya ulevi uliokithiri yani kulewa mpaka asubuhi na huendelea siku inayofuata mfululizo.

Kila wakati anaomba msamaha kubadilika hali ni ile ile. Kwa wazoefu unahisi anaweza kubadika au kwenye Ndoa vitendo vitazidi. Nimevumilia yapata miaka miwili now lakini bado tabia ipo.
LEWA ZAIDI YAKE
 
Dawa nzuri tafuta kwanza sababu inayomfanya anywe pombe. Kisha ndo umpe dawa
 
Attachments

  • 1717236952349.jpg
    1717236952349.jpg
    92.6 KB · Views: 3
Suala la kuacha pombe ni maamuzi ya mnywaji kuacha.
Nilikuwa na mtu wangu wa Karibu alishindwa kuvumilia unywaji wa mume wake nae akasalenda ndoa na kuondoka na watoto wake matokeo mume nae aliekuja kupoteza kazi maana pombe ilifika Hadi ofisini. Shortly, kuwa mvumilivu ishi nae unapoweza kumsaidia msaidie, usimkatie tamaa IPO siku atafanya maamuzi binafsi ya kuacha.
 
kwa kweli swala la pombe ni swala gumu sana,

kwanza anatumia pombe gani?? ni beer au hizi kali za kwenye plastiki za siku hizi???

je anaweza kufanya kazi zake? kama ni beer tu anakunywa basi huyo bado hana matatizo sana ila kama ameshaingia kwenye hizi za kisasa za akina kisungura basi hapo anahitaji sala na maomnbi ya kutosha
Anatumia zote beer na hizi kali. Ubaya zaidi anatumia pesa nyingi Bar zaidi ya laki tano na kuendelea Akilewa kurudi asubuhi kwa uzoefu wenu wadau je swala la ndoa hapa litawezekana au nirudi kwetu Marangu? Je anaweza kubadilika kama anavyosema🥲🥲
 
Naomba ushauri.

Nina mwanaume wangu lakini ana tabia ya ulevi uliokithiri yani kulewa mpaka asubuhi na huendelea siku inayofuata mfululizo.

Kila wakati anaomba msamaha kubadilika hali ni ile ile. Kwa wazoefu unahisi anaweza kubadika au kwenye Ndoa vitendo vitazidi. Nimevumilia yapata miaka miwili now lakini bado tabia ipo.
Akiwa kalewa hajitambui chukua yai la kuku lipasue halafu mwagia ute kiasi katikati ya matako uone kama ataendelea kulewa
 
Bila shaka wewe ni Mkibosho kama huyo mumeo.

Huyo ni mlevi tu kama walevi wengine. Usitarajie abadilike.

Achana naye mapema.

Huko Kibosho kuna walevi wengi na hawaambiliki.
 
Anatumia zote beer na hizi kali. Ubaya zaidi anatumia pesa nyingi Bar zaidi ya laki tano na kuendelea Akilewa kurudi asubuhi kwa uzoefu wenu wadau je swala la ndoa hapa litawezekana au nirudi kwetu Marangu? Je anaweza kubadilika kama anavyosema🥲🥲
Hebu jaribu kumwacha kwa majaribio uone kama atashituka...unaweza kuja kukaa kwangu kwa wiki nzima!!!
 
Wewe mwenyewe Mushi.. akina mangi wote wako hivo.... Vp kitimoto anatumia??? Bila shaka na hiyo nayo ndio mambo ya kibosho, marangu na rombo huko
 
Back
Top Bottom