Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa Obama kumlinda mwandishi

Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa Obama kumlinda mwandishi

walijua kabisa kwamba policcm intelijensia yao ni sufuri, sana sana wangewaharibia , wakawapiga chini.
Hii mi policcm ovyoo kabisa,yaani pamoja na kupelekwa Marekani kozi kwa makundi enzi ya IGP aliyepita akili zao zinawaza-ulinzi shirikishi,utii bila shuruti,kubambikia watu kesi na jioni kulewa pombe,utadhani sala ya kila siku,we mwite polisi yeyote afandee mwone atakavyokwitikia' UTII BILA SHURUTI EEEH'.Utadhani alikuwa usingizini.
 
Jana nilikuwa pale IFM wakaja FFU mbona walizuiwa kuingia pale makumbusho hata baada ya kuuingia bado walikaguliwa na MBWA wa wanausalama wa Marekani
 
Mwandishi wa Gazeti Uhuru anayejulikana kwa jina Selina Wilson alienda makumbusho ambako kulikuwa na ugeni mzito wa Mke wa Obama Michelle Obama kwa mwenyeji wake Salma Kikwete. Selina alikuwa na kitambulisho kilichoonyesha kuruhusiwa Symbion, lakini jina lake lilikuwepo kwenye orodha ya pale Makumbusho.

Kiongozi wa usalama Tanzania alimtilia nguvu mwandishi Selina Wilson na kumsukuma kwa nguvu atoke kwamba kitambulisho chake hakiruhusu kuingia pale ingawa jina lake lipo.

Mwanausalama wa Marekani aliingilia kati na kumwambia mwanausalama wa Tanzania kosa la kitambulisho si hoja ya kumfukuza kwa nguvu kwa sababu jina lake limo kati ya waandishi wa habari walioruhusiwa kuwepo pale.

Mwanausalama wa Marekani alienda mbali zaidi kwa kumwambia:
"Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu"? Mwanausalama huyo wa Obama alikasirishwa sana na kitendo kile cha udhalilishaji kilichofanywa na mwanausalama wa Tanzania, akaamua mwandishi Selina Wilson aingie kufanya kazi yake kwa vile jina lake lipo.

Tukio hili ni la aibu sana kwa wanausalama wetu walivyo wanyanyasaji kwa wananchi na vyombo mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari nchini.


Chanzo: http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/13683-rais-oboma-atua-dar-na-familia-kwa-kishindo

Huyu Mwanausalama wa US Angemsikia Pinda na kauli zake angezimia kabisa. Nchi hii ingawa inasingiziwa kuwa nchi ya amani, Ina manyanyaso mengi sana kwa Rai na Waandishi wa Habari.
 
Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu? Haya ni maneno mazito sana kuhusu maafisa wa usalama wetu.

Yap, ndivyo wanavyofundishwa, kutumia maguvu bila akili.

Rejea kauli ya waziri mkubwa wa Tanzania, "ukiambiwa usifanye hiki na wewe husikii, unajiona wewe ndio wewe, wewe ndiye jeuri, utapigwa tu, na mimi ninasema wawapige tu,maana hakuna namna nyingine, tumechoka sasa''.

Mkuu, fikiria waziri mkuu anasema hakuna namna nyingine inayoweza kuwa mbadala badala ya kupiga tu.

Sio kosa la huyo mwanausalama, ndivyo serikali inavyowafundisha kufanya.
 
Chama,
Tofauti ya hapa (Marekani) na nyumbani ni kwamba unaweza kumburura polisi aliyetumia nguvu mahakamani na kupata haki yako. Kwa Tanzania hiyo ni ndoto. Hapa polisi anapoua anapelekwa administrative leave immediately na upelelezi kufanyika. Nyumbani anapandishwa cheo. Sijadakia chochote.

Hayo ni yote nayaelewa hoja ni matumizi ya nguvu je unakubali hata hapa US yapo? Matokeo ya baadaye nini kinafanyika tutayajadili; mada kuu ni matumizi ya nguvu sasa kama unakiri yapo waleleze makamanda kwasababu wengi wao wamejenga hoja kana kwamba hivyo vitu havifanyiki hapa USA!
 
Maadam ni wa gazeti la uhuru, angeuwawa tu, make huwa wanawasifia polisi wanapovunja maandamano ya chadema.
 
Hayo ni yote nayaelewa hoja ni matumizi ya nguvu je unakubali hata hapa US yapo? Matokeo ya baadaye nini kinafanyika tutayajadili; mada kuu ni matumizi ya nguvu sasa kama unakiri yapo waleleze makamanda kwasababu wengi wao wamejenga hoja kana kwamba hivyo vitu havifanyiki hapa USA!
Matumizi ya nguvu yapo lakini yana tiba yake. Ingekuwa hapa Marekani leo Kamhunda asingepandishwa cheo. Angepelekwa mahakamani na kama si kufungwa jela angelipa fidia ya mamilioni kwa familia ya Mwangosi.
 
Sioni tofauti kati ya hao waandishi na hao mapoliccm kwasababu wote hujifanya wao simiongoni mwetu watanzania tunaonyanyasika kila kukicha WAACHENI WAFU WAZIKANE WENYEWE
 
Matumizi ya nguvu yapo lakini yana tiba yake. Ingekuwa hapa Marekani leo Kamhunda asingepandishwa cheo. Angepelekwa mahakamani na kama si kufungwa jela angelipa fidia ya mamilioni kwa familia ya Mwangosi.

Unachanganya mada! matumizi ya nguvu yapo pande zote sasa waeleze makamanda kwamba hali hiyo hata huku ipo tena huku imechanganywa na ubaguzi sasa waelemishe makamanda halafu turudi kwenye adhabu na hatima za wahusika wanaotumia nguvu!
 
Hivi huwa wanafundishwa wapi?

.......Kwenye Msitu wa Mabwepande chini ya Mtaalamu wa mambo ya usalama kutoka CCM, Bwana Nchemba. Huwa wanapewa mafunzo ya kutumia maguvu kukabiliana na mambo yasiyohitaji nguvu, jinsi ya kung'oa meno na kucha bila ganzi, jinsi ya kutoboa macho bila ya kuziathiri kope, kumwagia watu tindikali na kutumia poronium kuwadhuru viongozi wao wenyewe.

BIG UP!! kwa Lameck Madelu Nchemba matunda ya mafunzo yako yameonekana leo kwa huyo mwanishi wa habari
 
mi kila siku nasema tanzania police no manners😛ainkiller:😛ainkiller:
 
TISS ni nzuri ila tatizo inatumia WINDOWS 98 wakati dunia ya leo iko windows 8... madhara yake ndo hayo sasa..
 
Huyu Mwanausalama wa US Angemsikia Pinda na kauli zake angezimia kabisa. Nchi hii ingawa inasingiziwa kuwa nchi ya amani, Ina manyanyaso mengi sana kwa Rai na Waandishi wa Habari.

Hiyo signature yako kiboko... Dhaifu alijiumbua "live". Kama lugha si yako si uiache? Wakalimani mbona wapo? Rais wa China kaongea Kichina. Wewe wamjibu Kiingereza. Yaani wathamini Kizungu kuliko Kiswazi? Duuuuuu!
 
Aibu!, Aibu!, another thing an american was shocked was to see tht moron push and use such force on a WOMAN!

Arizona state troopers WA kiume wameshtakiwa kumkagua maeneo nyeti WOMAN wakitafuta bangi.
 
Back
Top Bottom