Hii mi policcm ovyoo kabisa,yaani pamoja na kupelekwa Marekani kozi kwa makundi enzi ya IGP aliyepita akili zao zinawaza-ulinzi shirikishi,utii bila shuruti,kubambikia watu kesi na jioni kulewa pombe,utadhani sala ya kila siku,we mwite polisi yeyote afandee mwone atakavyokwitikia' UTII BILA SHURUTI EEEH'.Utadhani alikuwa usingizini.walijua kabisa kwamba policcm intelijensia yao ni sufuri, sana sana wangewaharibia , wakawapiga chini.
CCP Moshi - Kilimanjaro na Kamishna wa Mafunzo ni CP Paul Chagonja
Mwandishi wa Gazeti Uhuru anayejulikana kwa jina Selina Wilson alienda makumbusho ambako kulikuwa na ugeni mzito wa Mke wa Obama Michelle Obama kwa mwenyeji wake Salma Kikwete. Selina alikuwa na kitambulisho kilichoonyesha kuruhusiwa Symbion, lakini jina lake lilikuwepo kwenye orodha ya pale Makumbusho.
Kiongozi wa usalama Tanzania alimtilia nguvu mwandishi Selina Wilson na kumsukuma kwa nguvu atoke kwamba kitambulisho chake hakiruhusu kuingia pale ingawa jina lake lipo.
Mwanausalama wa Marekani aliingilia kati na kumwambia mwanausalama wa Tanzania kosa la kitambulisho si hoja ya kumfukuza kwa nguvu kwa sababu jina lake limo kati ya waandishi wa habari walioruhusiwa kuwepo pale.
Mwanausalama wa Marekani alienda mbali zaidi kwa kumwambia:"Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu"? Mwanausalama huyo wa Obama alikasirishwa sana na kitendo kile cha udhalilishaji kilichofanywa na mwanausalama wa Tanzania, akaamua mwandishi Selina Wilson aingie kufanya kazi yake kwa vile jina lake lipo.
Tukio hili ni la aibu sana kwa wanausalama wetu walivyo wanyanyasaji kwa wananchi na vyombo mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari nchini.
Chanzo: http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/13683-rais-oboma-atua-dar-na-familia-kwa-kishindo
Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu? Haya ni maneno mazito sana kuhusu maafisa wa usalama wetu.
Chama,
Tofauti ya hapa (Marekani) na nyumbani ni kwamba unaweza kumburura polisi aliyetumia nguvu mahakamani na kupata haki yako. Kwa Tanzania hiyo ni ndoto. Hapa polisi anapoua anapelekwa administrative leave immediately na upelelezi kufanyika. Nyumbani anapandishwa cheo. Sijadakia chochote.
Matumizi ya nguvu yapo lakini yana tiba yake. Ingekuwa hapa Marekani leo Kamhunda asingepandishwa cheo. Angepelekwa mahakamani na kama si kufungwa jela angelipa fidia ya mamilioni kwa familia ya Mwangosi.Hayo ni yote nayaelewa hoja ni matumizi ya nguvu je unakubali hata hapa US yapo? Matokeo ya baadaye nini kinafanyika tutayajadili; mada kuu ni matumizi ya nguvu sasa kama unakiri yapo waleleze makamanda kwasababu wengi wao wamejenga hoja kana kwamba hivyo vitu havifanyiki hapa USA!
Matumizi ya nguvu yapo lakini yana tiba yake. Ingekuwa hapa Marekani leo Kamhunda asingepandishwa cheo. Angepelekwa mahakamani na kama si kufungwa jela angelipa fidia ya mamilioni kwa familia ya Mwangosi.
Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu? Haya ni maneno mazito sana kuhusu maafisa wa usalama wetu.
Hivi huwa wanafundishwa wapi?
Mkuu yaani hilo ni tusi zito sana.Duh!
Huyu Mwanausalama wa US Angemsikia Pinda na kauli zake angezimia kabisa. Nchi hii ingawa inasingiziwa kuwa nchi ya amani, Ina manyanyaso mengi sana kwa Rai na Waandishi wa Habari.
Aibu!, Aibu!, another thing an american was shocked was to see tht moron push and use such force on a WOMAN!