Mwandishi aliyeandika tuhuma za RC Simiyu adaiwa kukamatwa na Polisi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
20240614_083636.jpg

Kuna taarifa za kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari, Dinna Maningo ambae pia ni mmiliki wa Dima Online aliyechapisha kwa mara ya kwanza taarifa ya tuhuma za aliyekuwa RC Simiyu kulawiti, mwandishi huyu amekamatwa Tarime usiku wa kuamkia Juni 13, 2024.

Taarifa za awali zinadai kuwa mwandishi huyu kakamatwa Tarime mkoani Mara na Askari kutoka mkoa wa Mwanza na amesafirishwa kwenda Mwanza .

Matukio Daima Media inamtafuta RPC wa Mara na Mwanza kwa taarifa kamili.

CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA

============

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa amesafirishwa kwenda Mwanza lakini Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko amesema “Ni kweli tumejulishwa kuwa baada ya kukamatwa akiwa Tarime walitaka kumleta Mwanza na wakati wanaondoka naye wakasema wanamleta Mwanza ila huku hajafika, inavyoonekana yupo hukohuko Tarime.”

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob amesema “Alikamatwa na Askari Polisi, jana jioni majira ya Saa Mbili Usiku (Juni13, 2024), akafikishwa Kituo cha Polisi Tarime, nilionana na Dinna lakini alikuwa hajaambiwa kosa lake ni lipi.”

JESHI LA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, SACP Mark Njera hajapatikana kuzungumzia kinachoendelea.

=================

Mara Press Club yaliomba Jeshi la Polisi Mwanza kuweka wazi tuhuma za mwandishi wa habari Dinna

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) imeliomba Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuweka wazi tuhuma zinazomkabili mwandishi wa habari wa blogu ya Dima Online, Dinna Maningo.

“Tuna imani Jeshi la Polisi mkoani Mwanza litatoa taarifa kuhusu tuhuma zinazomkabili mwandishi na mwanachama wetu wa Mara Regional Press Club, ndugu yetu Dinna Maningo bila kuchelewa," Mwenyekiti wa MRPC, Mugini Jacob amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Juni 14, 2024.

Jacob amesema Dinna alikamatwa nyumbani kwake mjini Tarime, Mara jana majira ya saa mbili usiku na hadi leo mchana alikuwa anashikiliwa katika kituo cha polisi Tarime

“Mara tu baada ya kukamatwa kwa Dinna nilipata taarifa na nilifika kituo cha polisi Tarime, tukaonana, alikuwa vizuri lakini aliniambia polisi waliomkamata hawakumwambia sababu ya kumkamata," Jacob amesema kwa kifupi.

Jacob amesema leo Ijumaa pia amefika katika kituo cha polisi Tarime na kuonana na Dinna ambapo amemueleza kuwa askari polisi waliomkamata wamemwambia wanamsafirisha kwenda jijini Mwanza wakati wowote kuanzia sasa.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo amesema MRPC inawasiliana kwa karibu na uongozi wa Mwanza Press Club ili kusaidiana kufuatilia tukio hilo.

“Tuna imani jeshi letu la polisi litafanya kazi yake kwa weledi ili haki iweze kutendeka kwa wakati," amesema Jacob.

Chanzo: maraonlinenews

==================

WhatsApp Image 2024-06-14 at 15.02.50_d15f8c1a.jpg

=====

Pia soma

~MCL: Mkuu wa Mkoa adaiwa kumlawiti mwanafunzi wa SAUT
~Hii kamatakamata ya Waandishi wa Habari na ukimya wa Polisi, ni hatari kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari
 
Kuna taarifa za kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari, Dinna Maningo ambae pia ni mmiliki wa Dima Online aliyechapisha kwa mara ya kwanza taarifa ya tuhuma za aliyekuwa RC Simiyu kulawiti, mwandishi huyu amekamatwa Tarime usiku wa kuamkia Juni 13, 2024.

Taarifa za awali zinadai kuwa mwandishi huyu kakamatwa Tarime mkoani Mara na Askari kutoka mkoa wa Mwanza na amesafirishwa kwenda Mwanza .

Matukio Daima Media inamtafuta RPC wa Mara na Mwanza kwa taarifa kamili.

CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA
Duh...!, hizi mambo zimeanza tena?!..., au Maza nae anaelekea kuwa like Maza like Faza?!.
Tusubirie taarifa ya Edwin Soko wa MPC, kuthibitisha hao waliomkamata ni polisi kweli... maana... Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
P
 
Kuna taarifa za kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari, Dinna Maningo ambae pia ni mmiliki wa Dima Online aliyechapisha kwa mara ya kwanza taarifa ya tuhuma za aliyekuwa RC Simiyu kulawiti, mwandishi huyu amekamatwa Tarime usiku wa kuamkia Juni 13, 2024.

Taarifa za awali zinadai kuwa mwandishi huyu kakamatwa Tarime mkoani Mara na Askari kutoka mkoa wa Mwanza na amesafirishwa kwenda Mwanza .

Matukio Daima Media inamtafuta RPC wa Mara na Mwanza kwa taarifa kamili.

CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA
Kakamatwa kwa sababu zipi?
 
Wanaharakati waingie kazini
 
Ataachiwa Kama Hakuna kosa alilofanya. Unyanyasaji wa Kijinsia bado ni janga sana!
 
Kitoto cha chuo chenyewe ni kishenzi, kikafanyiwa ushenzi, ajabu jamii inalalamika, kale simply kalikutana na ajali kazini kakiwa kwenye mihangaiko yake.

Katoto mpaka kanaamua kuripoti polisi itakuwa kalitaka kupandishiwa dau la kusuguliwa nyuma, jamaa akakataa ndio kakaamua kwenda polisi, naamini kama kangepewa pesa ya huduma ya nyuma kangeendelea kucheka cheka tu.
 
Back
Top Bottom