Mwandishi Munga Tehenan: YUPO WAPI?

Mwandishi Munga Tehenan: YUPO WAPI?

Ni kweli alitangulia. Na baada ya hapo gazeti la Jitambue nalo lilianza kupotea.
 
Binafsi nilikua nafanya nae kazi. Pia alinsaidia kuniongezea ujuzi na weledi na moyo wa kuandika. Kuhusu kuenziwa naamin baadhi ya watu ambao wangeongoza kumuenzi ni wanafiq wa kubwa. Wanahisi wangemtangaza zaidi. Unajua wengi wamezoea kukandamiza sifa za watu. RIP Munga Tehnan. Na falsafa zake za EGOiSM.
 
Kuna thread ilishaletwa humu JF in 2009/10 i hope itapatikana ziunganishwe
 
Kabla ya kuachana na mwili, katika siku zake za mwisho yeye pamoja na waliokua wasomaji wa gazeti la Jitambue waliasisi taasisi iinayoitwa JITAMBUE FAMILY AU FAMILIA YA JITABUE. Taasisi hiii inafundisha ''elimu ya utambuzi''.

Baadhi ya masomo yanayofundishwa na taasisi hii ni: Mwili wa hisia, werevu wa hisia, kujihamini na kutojihamini, uhusiano na wengine, kuishi na wakorofi, njia za kujizoeza kujikubali, malengo, tahajudi, kanuni za mahumbile, nguvu za ziada, machale, ndoto na uchawi. Haya ni baadhi ya masomo ambayo alikua akiyafundisha enzi za uhai wake. baadhi ya haya masomo yamerokudiwa unaweza kupata cd zake au video.

Kama unahitaji kujua zaidi kuhusu upatikanaji wa habari zake ikiwamo na vitabu alivyoviandika tuwasiliane nikuelekeze. Piga simu 0717114409.
 
habari hii imenisikitisha sana , nilikuwa sijui kama Munga wa gazeti la jitambue alikufa. mke wangu (enzi hizo akiwa girlfriend) alikuwa anapenda sana magazeti yake... nimemwambia katoa machozi!! nitakupigia
 
<b>Kwa hakika, inaumiza sana kwamba alipofariki hakuna hata makala moja iliyoandikwa juu yake na waandishi wenzake. kama ipo, nipo tayari kukosolewa. Ametutoka kimya kimya mno kwa mtu aliyekuwa na jina kubwa katika sanaa ya habari kama yeye. Mdau uliyeleta makala ya Munga umenishitua sana kwamba hata kwenye msiba wake kulitokea mambo kama aliyoandika. Inasikitisha</b>.
<br />
<br />




Hata Mimi sielewielewi ninayoyasoma hapa,Munga Tehenan anawezaje kufa halafu habari yake iwe siri? Media haiku-cover habari hii?
Mm amenisaidi sana,Tehenan nilikuwa sikosi Gazeti la Jitambue,hata siku moja sikosi!!
Amenisaidia saaana,i never thot kwamba hatunaye kimwili tena,duuuuh!!!
2008 ni Mwaka Juzi tu,ama kweli Media za Bongo ni zaidi ya huzijuavyo!!!
 
jamaa alishafariki kitambo
..Wadau naomba kujuwa alipo mwandishi maarufu wa makala ,na one time mhariri na mmiliki wa gazeti la JITAMBUE...ameandika vitabu vingi vya lugha na hadithi...na kuna wakati alikuwa na TALK SHOW pale TBC1 Wakati ikiwa TVT........pia amewahi kuwa majira publishers..nadhani mharriri wa vitabu..among other things...

..MHARIRI ..MUNGA TEHENAN....
 
RIP Munga, nazikumbuka sana makala zako kwenye gaziti la 'Jitambue'.

Munga ni mmoja ya watu ambao wananifanya nitamani kuwapo kwa teknologia ambayo binaadamu tunaweza ku'copy' kumbukumbu kutoka kwa mtu mmoja na kuhamishia kwa mtu mwingine au tu kuzihifadhi (I mean to copy intelligence from a person before he dies so that we can later on paste into one or more other living persons or access it for other uses).

Rest in peace Munga Tehenan.
 
Rest in Peace Munga Tehanan, Nakumbuka kazi zetu za Mwisho tulizo fanya pamoja na Ushauri wako ulio nipa juu ya Kitabu changu kilicho nyimwa ithibati pale Wizara ya Elimu. Nakumbuka uliniambia. Vitabu vingine pale vinapewa ithibati bila hata kupitiwa. Inategemea tu how you play the dice.

You were a cool man.
 
Tehenani alikuwa kichwa mi alinifanya nikabadili mambo mengi sana, nakumbuka nilikuwa nafanya kazi sehemu, boss alikuwa mkorofi mshahara kutoa mbinde kuacha kazi nilikuwa naogopa, akaniambia kuwa natumika bure kwa sababu ya hofu yangu, akaniambia ingekuwaje kama huyo boss angekuwa amekufa na ajira hakuna tena, akasema nichukulie boss kafa na niache kazi, kweli nikaacha nikatafuta nyingine na ndiyo ninayo mpaka sasa
 
R I P Munga
Kiukweli mafundisho yako ndio yaliyoniongoza sana kiasi kwamba leo hii sitetereki kabisa,
Nimekuwa sio mtu wa kuongozwa na hisia bali mimi ndio huongoza hisia zangu.
 
Back
Top Bottom