Mwandishi wa Habari, Kazimbaya Makwega ashikiliwa na Polisi, asafirishwa kutoka Mwanza hadi Dodoma

Mwandishi wa Habari, Kazimbaya Makwega ashikiliwa na Polisi, asafirishwa kutoka Mwanza hadi Dodoma

Journalist Arrested in Mwanza for Publishing ‘False’ News About UDOM​


UDOM criticisms

Police also were not specific about what information about UDOM that Makwega has published was “false.” In his blog, Mr Makwega has published several articles that spotlight the mismanagement of UDOM that led to the poor academic performance of many students.

The blogger’s articles also accused UDOM’s top leadership of being “irresponsible” for failing to take time and listen to the university’s students and find ways to address their issues and concerns.

In his most recent article, published on February 19, 2024, Makwega accuses UDOM chancellor Stergomena Tax of “failing” to protect young girls at the university from acts of sexual corruption, which he claims to be “rampant.” Dr Tax also serves as the Minister of Defence and National Service.

He gives an example of a young girl who told her father about her plan to drop out of college because a certain lecturer won’t let her study in peace as he regularly asks her to sleep with him.

READ MORE
Source: TheChanzo.com
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Salama Wana JF, Nimeona andiko hili huko Mtandaoni, kuna mwenye taarifa ya kinachoendelea?
View attachment 2913618
===

Mwandishi Kazimbaya Makwega asafirishwa toka Mwanza kwenda Dodoma

Ndugu waaandishi wenzangu muda huu nimefika kituo kikuu cha polisi kati na mawakili wa wawili wa OJADACT kufuatilia kukamatwa kwa Mwandishi wa habari kazimbaya makwega.

Kwa bahati nzuri tumemkuta hapa kituoni na nimepata nafasi ya kuongea naye ana kwa ana kama dakika 5 hivi.

Wakati naongea naye wakaja maafisa waliojitambulisha kuwa wanatoka ofisi ya RCO Dodoma na wamekuja kumchukua ili waondoke naye.

Nao pia walikubali kuongea na mimi pia na sio mawakili nami nikafanya hivyo tukaongea na wakaniambia wanaondoka naye kwenda dodoma saa 7 mchana.

Pia wakasema kuna tuhuma huko Dodoma za kujibu hivyo tuwe na amani kwani hizo ni tuhuma.

Hapo nikawauliza kuwa kama.wanatoka Dodoma mbona tumeongea na ofisi ya RPC dodoma na ikathibitisha kuwa hakuna askari wake waliokuja Mwanza.

Wao wakajibu kuwa ofisi ya RPC ni kubwa ila wao wanatoka ofisi ya RCO Dodoma.

Maelezo toka kwa makwega mwenyewe ni kuwa alikamatwa jana kwao Malya na akanyang'anywa laptop na simu zake tatu na pia alipofika hapa kituoni akaandikishwa maelezo.

Gari yenye namba za usajili SU 45605 landCruiser imeondoka na Makwega hapa kituo cha polisi kati Mwanza.

Maelezo ya mwisho toka kwa watu wanaomshikilia walisema wataondoka saa 7 mchana ila kwa sasa wanaenda wapi ? Hatujajua na ilikuwa ngumu kuhojji.

Afya ya Makwega
Ipo salama kabisa nilipoomba tumpe kwanza chai anywe wakasema watampa wao na hiyo ni haki yake kama binadamu hivyo watamhudumia.

Naomba wemzetu mlioko Dodoma jipangeni kwa ajili ya kumpokea .

Ushirikiano na Jeshi la polisi.
Tangia nilipofika kituoni nimepata ushirikiano mzuri na nilipojitambulisha wakamruhusu niongee naye kwa kina.

Ahsanteni sana wote

Edwin Soko
Mwenyekiti
OJADACT
MPC .


================

MAELEZO YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mwanza, Edwin Soko ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (OJADACT) anasimulia:

Taarifa nilizipata ni kuwa akiwa Chuo cha Mallya Wilayani Kwimba (Mwanza), jana Februari 22, 2024, alifuatwa na maafisa waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi wanatoka Ofisi ya RPC Dodoma.

Wakaenda naye hadi nyumbani kwake lakini walionana pia na Mwneyekiti wa Serikali za Mtaa, wakaanza ukaguzi, kutokana na ukaguzi huo wakachukua laptop yake moja na simu mbii.

Wakamwambia kesi yake ipo Dodoma, wakamwambia anatuhumiwa kuandika habari za uchochezi kuhusu Chuo Kikuu cha Dodoma.

Wakamsafirisha hadi Mwanza. Asubuhi ya leo (Februari 23, 2024) nilifika katika Kituo cha Polisi Mwanza, nikaomba kuonana naye, wakaniruhusu kuonana naye.

Nikazungumza na Makwega akaniambia wamemshikilia kwa madai ya kuandika habari ya uchochezi kuhusu UDOM.

Tukiwa tunaendelea na mazungumzo wakaja maafisa wengine ambao walijitambulisha kuwa wao ndio waliomchukua kutoka nyumbani kwake.

Nilipowauliza kuwa mnatoka Ofisi ya RPC lakini nimezungumza na RPC wa Dodoma kasema yeye hana taarifa, wakasema “Ofisi ni kubwa sana, wao wanatoka Kitengo cha RCO”.

Hivyo, wakasema wataondoka naye saa saba mchana (leo Februari 23, 2024) kwenda Dodoma, baada ya hapo hatujui nini kilichoendelea.


RPC DODOMA AKIRI KUKAMATWA KWA KAZIMBAYA MAKWEGA
Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amesema:

Amekamatiwa Mwanza, kuna tuhuma dhidi yake zinazomkabili, anamiliki blog inayoitwa ‘Mwanakwetu’, inasemekana ametumia mtandao vibaya, watu wa kitengo cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wamemfungulia mashtaka ya kutumia mtandao vibaya.

Kuna vitu ambavyo aliandika akituhumu hicho chuo, hivyo amekamatwa ili aandike maelezo na taratibu nyingine za kipelelezi zitaendelea na ikithibitika kuna kitu ambacho amekutwa nacho taratibu nyingine zitaendelea.

Anasafirishwa kutoka Mwanza kuja Dodoma kwa ajili ya kutoa maelezo zaidi na taratibu nyingine za Kipolisi.

UTPC WASEMA WANAFUATILIA MCHAKATO
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya anasema:

Ni kweli amekamatwa tumepata taarifa hizo, amekamatiwa Mwanza na anasafirishwa kwenda Dodoma, kuhusu tuhuma hasa hatujajua, tunasubiri afikishwe Dodoma kisha taratiu nyingine zitaendelea, kwa sasa ni hayo tu.
Kalamu za waandishi wa habari wa Tanzania zimefungwa ving'amuzi, write at your own risk, bosi mkuu anasema wewe andika yote sisi tutachukua yanayotuhusu.
 
Raia hawana thamani mbele ya Watawala kabisa wanamsafirisha mtu mpaka Dodoma kwa ishu za kijinga jinga tu na kuacha mambo ya Msingi...
Ila ukipata utapeli wa kimtandao unaambiwa utoe 50,000 ya kumtrack , then mwizi akijulikana aliko unaambiwa uwawezeshe Askari wakamkamate songea.

Unawapa uwezeshaji anafikishwa wanaanza story bado tunachunguza kaachiwa kwa dhamana, afu unakuta mplelezi wa kesi yako na mtuhumiwa wanalewa meza moja jioni. Tuombe Rehema za Mungu, Mbingu Ngumu mnooo
 
kama yuko mikono salama ya jeshi la polisi nafikiri hakuna shida
 
Arresting inafanyika wakati docket imeshafunguliwa,upelelezi umeshafanyika na DPP amesha apply mind kuwa ana winnable case, sasa hii naona ni kinyume kabisa, na hope's wakati wa Arresting walimtajia haki zake
 
Back
Top Bottom