TANZIA Mwandishi wa habari wa TBC Joachim Kapembe amefariki dunia

TANZIA Mwandishi wa habari wa TBC Joachim Kapembe amefariki dunia

Kuna Siri gani Kati ya kishuka mlima Kilimanjaro na kifo?. Kuna rafiki yangu naye alifariki wakati wanashuka mlima Kilimanjaro.
Hata vyombo vya anga za juu wakati wa kuitoka atmosphere hakuna shida kimbembe ni wakati wanatokea huko sasa kuingia kwenye blanket linaoitwa atmosphere ambapo ni kuanzia kilomita 40,000 ukiwa juu sasa uelekee duniani.
Na ndio maana hata vimondo huwa vinadondoka kila siku lakini havifui dafu vinaungua na kuwa majivu sisi huku hatuwezi jua lakini duniani kote vimajivu vinadondoka.
Chombo cha juzi tu cha Orion kilichokwenda mwezini ukikiangalia pale baharini kilipotua kimebabuka mno hebu tuchunguze hapa kulikoni
 
View attachment 2446256

Mwandishi wa habari wa TBC mkoani Manyara, Joachim Kapembe amefariki dunia Desemba 13, 2022 akishuka kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Kapembe aliungana na Waziri Nape Nnauye na viongozi wengine katika uzinduzi wa huduma ya intaneti kwenye kilele cha mlima huo.

Swahilitimes.
Uandishi wa habari wa sasa ni kama unasevu jina kwenye simu ya batani.... lazima uandike kwa ufupi iwezekanavyo.

Unasoma habari badala uhabarike unabaki na maswali
 
Bila shaka High altitude disease imeuondoa, apumzike kwa amani
 
Ila mbona kuna check point nyingi tu, na unapimwa kabla ya kuendelea na check point nyingine, kama hauko fit wanakushauri tu usiendelee.
 
Ila mbona kuna check point nyingi tu, na unapimwa kabla ya kuendelea na check point nyingine, kama hauko fit wanakushauri tu usiendelee.
Tatizo yeye alikuwa na Kazi ya kuripoti poa TBC zote,kind of fatique
 
Apumzike kwa aman.

Japo alikua yuko kazini Ila watu wasiwe wanaforce kupanda huo mlima bila kua na mazoezi ya kutosha, au unakuta mtu ana pressure na magonjwa yasiyoambukiza anataka nae akapande..

kuna stori iko humu kuhusu safari ya kupanda mlima,ukiisoma kwa utulivu hupandi huo mlima.

au unawezaenda ukaghairi njiani,maana wanaofariki sio mtu mmoja.
 
kuna stori iko humu kuhusu safari ya kupanda mlima,ukiisoma kwa utulivu hupandi huo mlima.

au unawezaenda ukaghairi njiani,maana wanaofariki sio mtu mmoja.
Nitautafuta, nilipanga mwakani nikapande panapo uzima. Ni dream yangu kupanda huu kwanza kabla ya Everest... ambao sina hakika kama nitarudi 😪
 
Apumzike kwa aman.

Japo alikua yuko kazini Ila watu wasiwe wanaforce kupanda huo mlima bila kua na mazoezi ya kutosha, au unakuta mtu ana pressure na magonjwa yasiyoambukiza anataka nae akapande..
... unywele mmoja ukishabadilika kuwa mweupe hizo mambo ni kuwaachia vijana wenye nguvu zao.
 
Ni wizi tu na roho mbaya yetu sisi watanzania lakini ilitakiwa kila kikosi cha wapanda mlima wasikose wataalamu wa afya ili kusaidia ku monitor afya za wapandaji na kutoa emergence care........
 
Nitautafuta, nilipanga mwakani nikapande panapo uzima. Ni dream yangu kupanda huu kwanza kabla ya Everest... ambao sina hakika kama nitarudi [emoji25]

tena aliyesimulia ni mwanamama kama wewe,hope utakujengea kujiamini zaidi[emoji122]
 
Back
Top Bottom