TANZIA Mwandishi wa habari wa TBC Joachim Kapembe amefariki dunia

TANZIA Mwandishi wa habari wa TBC Joachim Kapembe amefariki dunia

RIP, poleni mno kwa wafiwa na staff mates wake wote, mkuu ni haki yako kuchangia ila mimi hii issue nimeiona kwa upande wa pili, tumeshuhudia watu walio fit kabisa,gym kila siku na wana drop dead ndani ya gym, pia hapa kuna tatizo kubwa mno,uokoaji wetu pale mlimani bado ni wa kijima, nchi ilipata aibu mno kipindi kile yule celebrate kutoka SA alipofia mlimani wakati uzuzu ule unafanyika wa kumkimbiza chini kwa kutumia mkokoteni, Ile ni aibu na kama nchi hatujifunzi, juzi kati tumeionyesha dunia jinsi ya kuokoa ndege kwa kamba na mitimbwi!
Kwenda gym kumbuka upo level ile ile ila kupanda mlima kila siku elevation ina change na kadri unavyopanda kumbuka oxygen inapungua
 
Kuna Siri gani Kati ya kishuka mlima Kilimanjaro na kifo?. Kuna rafiki yangu naye alifariki wakati wanashuka mlima Kilimanjaro.
Msukumo wa damu ukiwa kileleni ni mkubwa kuliko unapokuwa huku chini, sasa kama hauko vizuri unapata mushkeli unapobadili mazingira.
 
Hata vyombo vya anga za juu wakati wa kuitoka atmosphere hakuna shida kimbembe ni wakati wanatokea huko sasa kuingia kwenye blanket linaoitwa atmosphere ambapo ni kuanzia kilomita 40,000 ukiwa juu sasa uelekee duniani.
Na ndio maana hata vimondo huwa vinadondoka kila siku lakini havifui dafu vinaungua na kuwa majivu sisi huku hatuwezi jua lakini duniani kote vimajivu vinadondoka.
Chombo cha juzi tu cha Orion kilichokwenda mwezini ukikiangalia pale baharini kilipotua kimebabuka mno hebu tuchunguze hapa kulikoni
Hapo kwenye Km 40,000, rekebisha, ni chini ya Km 400
 
Kilimanjaro the roof of afrika ni mlima niliopanda zaidi ya miaka Saba nilianza kupanda nikiwa darasa la sita nimebahatika kupanda njia zote katika njia hizo marangu rout au cokacola rout ni njia pekee yenye nyumba za kulala maji ya bomba na umeme wa Sola na ndio njia kongwe na ni njia ya gharama kuliko zote sema pia ndio njia hatari Kwa vifo kuliko zote hasa kutokana tabia ya Hali yake ya hewa kubadikabadika wakati wowote haswa kipande Cha kutoka horombo hut mpaka kibo hut hichi kipande unaweza kuamka uko fit na gafla ukaitwa marehemu hakina ujanja wa Jimu sijui mazoezi mlima ukikukataa hakuna namna hata kama ukiwa na madaktari bingwa utakufa tu nakumbuka Ile kipindi ya elnino mwaka 2000 nilishuhudia watu wawili wakikata roho na mzungu mmoja alikua daktari akijaribu kuwasaidia lakini ikashindikana mzungu akachanganyikiwa na yeye mwenyewe haelewi iacheni Kilimanjaro iitwe Kilimanjaro
 
Kuna Siri gani Kati ya kishuka mlima Kilimanjaro na kifo?. Kuna rafiki yangu naye alifariki wakati wanashuka mlima Kilimanjaro.
Kwa maeleo ya Gerson msigwa.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kifo cha Mwandishi wa Habari wa TBC Joachim Kapembe aliyefariki jana akiwa Mlimani Kilimanjaro kimetokana na ajali ya Baiskeli na sio madhara ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

"Nimesikitishwa sana na kifo cha Rafiki yangu
Joachim Kapembe tuliyekuwa nae kwenye
safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro, Kapembe
amefariki kwa ajali ya baiskeli wakati akitoka
katika kambi ya Kibo kuelekea kambi ya
Horombo baada ya kupanda mlima hadi kufika
kileleni kwa mafanikio na ni mmoja wa Watu
ambao hawakupatwa na madhara ya kupanda
mlima (mountain sickness)" --- Msigwa.

"Baada ya kufanikiwa kufika kileleni
Kilimanjaro na kushuka, Watu wote tulifika
kambi ya Kibo ambako tulipaswa kuendelea
kwenda kambi Horombo, wachache waliamua
kutumia baiskeli badala ya kutembea kwa
miguu akiwemo Joachim Kapembe bahati
mbaya akiwa anateremka mteremko wa
kutoka Kibo ndipo akapata ajali iliyosababisha
apoteze maisha"


"Natoa pole kwa Familia, Mkurugenzi Mkuu,
Wafanyakazi wa TBC, Waandishi wa Habari
wenzangu, ndugu jamaa na marafiki wote,
Mwenyezi Mungu amweke mahali pema
peponi... Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina
lake lihimidiwe, Amina" @gersonmsigwa
 
Back
Top Bottom