Kuna Siri gani Kati ya kishuka mlima Kilimanjaro na kifo?. Kuna rafiki yangu naye alifariki wakati wanashuka mlima Kilimanjaro.
Kwa maeleo ya Gerson msigwa.
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kifo cha Mwandishi wa Habari wa TBC Joachim Kapembe aliyefariki jana akiwa Mlimani Kilimanjaro kimetokana na ajali ya Baiskeli na sio madhara ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
"Nimesikitishwa sana na kifo cha Rafiki yangu
Joachim Kapembe tuliyekuwa nae kwenye
safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro, Kapembe
amefariki kwa ajali ya baiskeli wakati akitoka
katika kambi ya Kibo kuelekea kambi ya
Horombo baada ya kupanda mlima hadi kufika
kileleni kwa mafanikio na ni mmoja wa Watu
ambao hawakupatwa na madhara ya kupanda
mlima (mountain sickness)" --- Msigwa.
"Baada ya kufanikiwa kufika kileleni
Kilimanjaro na kushuka, Watu wote tulifika
kambi ya Kibo ambako tulipaswa kuendelea
kwenda kambi Horombo, wachache waliamua
kutumia baiskeli badala ya kutembea kwa
miguu akiwemo Joachim Kapembe bahati
mbaya akiwa anateremka mteremko wa
kutoka Kibo ndipo akapata ajali iliyosababisha
apoteze maisha"
"Natoa pole kwa Familia, Mkurugenzi Mkuu,
Wafanyakazi wa TBC, Waandishi wa Habari
wenzangu, ndugu jamaa na marafiki wote,
Mwenyezi Mungu amweke mahali pema
peponi... Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina
lake lihimidiwe, Amina" @gersonmsigwa