Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Mwandishi wa @MwananchiNews apotea. Siku 10 hajulikani alipo. Alikuwa anafanya uchunguzi wa Habari nyeti. Nataraji kesho tutajua zaidi - ZZK.

mwananchi.jpg


KUHUSU AZORY GWANDA
Azory Gwanda alizaliwa 1975 na alikuwa ni mwandishi wa habari wa Kampuni ya ya Mwananchi Communications iliyopo jijini Dar es Salaam.

Azory Gwanda alikuwa ana umri wa miaka 42 wakati wa kutoweka kwake. Gwanda alikuwa akiishi katika shamba karibu na Kibiti, Tanzania, na mkewe Anna Pinoni. Mama yake, Eva Mpulumba kutoka kijiji cha Msimba katika Mkoa wa Kigoma, aliishi na familia yake yote, lakini ndiye ndugu pekee aliyehojiwa kuhusu kupotea kwa Gwanda.

Wakati akifanya kazi katika Kampuni ya Mwananchi kama mwandishi wa habari wa kujitegemea, Gwanda aliandika mfululizo wa habari za mauaji yaliyokuwa yakitekelezwa huko. Inadhaniwa utekaji wake unahusiana na mfululizo wa habari za mauaji ambazo Gwanda alikuwa akiziandika.

Kupotea kwa Gwanda kumechochea mashirika mengi kujitolea kusimamia na kulinda haki za waandishi wa habari ulimwenguni kote. Haukupita hata mwezi mmoja baada ya kutoweka kwa Gwanda, shirika MISA Tanzania ilitoa tamko la kufadhaika kwao juu ya ukosefu wa taarifa kamili kuhusiana na kutoweka kwa Gwanda, na kukiita kitendo hicho kuwa "shambulio la uhuru wa waandishi wa habari ambalo lazima lihukumiwe"

Theophil Makunga, mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wa Tanzania, alisema watu wenye nia mbaya na Gwanda na taifa kwa ujumla walikuwa wakiendelea kufanya uovu wao hata kwa waandishi wa habari akiwemo Gwanda.

PIA, SOMA:
VISA DHIDI YA WANAHABARI WENGINE WA TANZANIA:
PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana

~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
"Nimehamia CCM baada ya kuona ilani za upinzani zinatekelezwa na Rais, hivyo nimehamia kwenye chama chake kuunga mkono".... WTF!!!!!!!!!!!!

Cluiser nyeupe tena? Huenda ni huyu ndo alivujisha issue ya kutekwa watoto 1300.
 
Watu wasiojulikana! Hahaha mwaka huu bora uishe tu
 
Mwananchi wenyewe hawajatoa taarifa ya hiyo habari nyeti kufuatiliwa!!

By the way kama alikuwa ni ripota wa magaidi basi watakuwa wamepotea naye.
 
Back
Top Bottom