Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

Mkuu nijuze ni akina nani hao wameondoka nae ama kumteka? daah Tanzania yetu ngoja niombe kwa Mungu kwa hisia kwanza
Chombo rasmi cha kutoa taarifa ni jeshi la polisi, tuwaache wafanye kazi yao.Ila ni vyema kwa wenye mapenzi mema na mustakabali wa taifa hili kufanya utafiti utakao leta ufahamu wa, ni taarifa gani alikuwa ameandika siku za usoni? Kuna habari,makala au ripoti iliyomchukiza mtu au watu wa mrengo fulani?Je huyu bwana ni muandishi wa sampuli ipi?
 
Wapinzan na waandishi hawahitajiki mmmmmh jaman ccm kwan hii ndo ccm mpya au mbona sielewiiiii
 
Wacha bana!!! anatumia jina gani humu? daah nouma kweli mi naenda Ifakara wameshavuna mpunga naenda kula pepeta na somba
Mkuu si vema kuweka hadharani privacy ya mtu na istoshe yupo kwenye matatizo huenda ikamletea matatizo zaidi. Kikubwa tumuombee tu ndugu yetu arudi salama.
 
A
_99102475_aa1e7a08-64e0-48d5-bc7a-bea59e3a1def.jpg


Image captionWafanyakazi wa kampuni ya Mwananchi walivalia mavazi meusi katika kikao na wanahabari
_99102478_azorybbc.jpg

Image captionMagazeti ya mwananchi leo yameongoza na kichwa cha habari [HASHTAG]#MrudisheniAzory[/HASHTAG]

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wanaamini kutoweka kwa mwandishi Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi kwa siku 17 sasa ni kwa nia mbaya.

Mwenyekiti ya jukwaa la wahariri Teofile Makunga anasema kama mwandishi huyu angekuwa anashikiliwa na vyombo vya usalama kwa sababu yoyote angetakiwa kuwa amefikishwa mahakamani kufikia sasa.

Mkurugenzi wa gazeti la Mwananchi Francis Nanai ameomba vyombo vya ulinzi na usalama kuzidisha kasi ya kumtafuta mwanahabari huyo ambaye ametoweka kwa zaidi ya siku kumi sasa.
Wahariri wanapanga kufanya maandamano ya kushinikiza kuzidishwa kazi kwa msako huo yatakayoanzia mnazi mmoja hadi makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali na kampuni ya magazeti ya mwananchi, mwanahabari huyo wa kujitegemea alitoweka tarehe 21 Novemba.

Bw Gwanda alikuwa anaishi na kuripoti kutoka mji mdogo uitwao Kibiti, ambao upo kilomita kama 130 hivi kusini mwa Dar es Salaam.

Bwana Gwanda ni mmoja wa waaandishi wa kwanza kabisa kuripoti kwa kina juu ya mfululizo wa mauwaji yaliyokuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana yaliyowalenga polisi na viongozi wa mji huo.

Mauwaji hayo yaliyotokea miezi kadhaa tu iliyopita yalitia hofu kubwa mjini hapo.

Mke wake Anna Pinoni alisema watu wapatao wanne wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walimchukua bwana Gwanda kutoka katikati ya mji huo, mahali ambapo hupendelea kukaa.

Anasema pia aliporudi nyumbani alikuta vitu vimezagaa, ishara kwamba inawezekana waliipekua nyumba yao.

Bw Azory aliwasiliana na ofisi za Mwananchi mara ya mwisho tarehe 20 Novemba kwa majukumu ya kikazi.
 
Back
Top Bottom