Mwandishi wa Watetezi TV mbaroni kwa madai ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni juu ya watuhumiwa kulazimishwa kulawitiana Kituo cha Polisi

Sipo upande wowote lakini kwa mtazamo wangu huyo mwandishi ana lake jambo na ninaweza kumuita yupo kundi la watu wanayoipinga serikali ya awamu ya nne na ndio maana yupo kwenye upande wa kuleta machafuzi, kwani alitakiwa atumie busara ya hali ya juu kwani hizo tuhuma zilikuwa ni kubwa sana. Anasema alifanyia uchunguzi je alishirikisha pia watuhumiwa? hata kama ingekuwa ngumu kwake kuwashirikisha je alishindwa kumshirikisha mkuu wa mkoa, tatizo la waandishi wa sasa hivi waliokosa maadili ya kiuandishi wanatabia ya kudharau mamlaka wanajifanya wao wamepitia taaluma ya kiuchunguzi au siku hizi chuo cha uandishi kina mafunzo hayo?.
 
Hawataki uovu wao ujulikane sio

Inashangaza, inahuzunisha na inafikirisha sana. Polisi ni watuhumiwa, wale vijana walalamikaji, Mwandishi ameweka hadharani malalamiko, Polisi ndiyo sehemu ya kupeleka malalamiko.

Ushauri: Walalamikaji ( mahabusu) wapeleke shauri mahakamani, Watuhumiwa (Polisi) waitwe kujibu hoja. Upelelezi ufanywe na JWTZ.

Tofauti na hapo, Walalamikaji (Mahabusu) na Shahidi (Mwandishi) watakuwa watuhumiwa kama shauri litashughulikiwa na Polisi.
 
Inakuwa vipi pale kesi ya mtuhumiwa inapo shughulikiwa na mtuhumiwa mwenyewe???
 
SASA kosa lake NINI?
Yeye amewahoji wahusika laivu bila Chenga kisha akatupia YouTube kila MTU aone.
Lingekuwa ni gazeti tungesema muongo, HAPO polisi mtaambulia aibu bure!.
 
Imebidi niitafute Nimeandika you tube WATETEZI TV yani habari imekuja kama yote. Sasa huyu muandishi mbona aliongea mpaka na kamanda wa polisi wa mkoa. Na amesema wako kwenye uchunguzi labda kutakua na shida nyingine who knows
 
Ikiwa hizo tuhuma ni za kweli maana najua kama ni uongo amefanya kosa,je kisheria atakua ana kosa?kisheria lakini tuweke hisia na mitazamo yetu pembeni maana naona umeshaanza kusema hadi ana watu nyuma yake sasa sijui hayo umeyajulia wapi.
 
Polisi wetu hawa niuchuro.kabisa
 
Waliofanyiwa ukatili huo wahojiwe mubashara na vituo vya luninga ( television) ili Watanzania wajue nani anstahili kuadhibiwa.
Acheni kuleta usisiemu kwenye profesheni ya polisi
 
Jwtz hawana ujuzi wa kupeleleza, hii kazi wanaweza maafisa usalama(TISS) na polisi wenyewe.Na kwa hapa Tz polisi ndio 'wajuvi wa upele'.
 
. POLICE ni watuhumiwa, kitendo cha mtuhumiwa kumkamata mtuhumu ni kuficha ushahidi. Ilitakiwa ukamataji ufanywe kwa kituo kinachotuhumiwa. Baadae ikibainika kuna kuna ushahidi wa kutosha iende mahakamani. Lakini hii si kwa Tanzania.
 
Police tukubaliane mapema..tunaanzia kwenye uraia au turuke moja kwa moja kwenye uhujumu uchumi?
#MembeSemaNeno#
#MwagaPombe2020#
Au tufanye utakatishaji fedha.

Au mabeberu yanamtumia kuchafua nchi.

Kweli nimeamini baba akiwa poyoyo na watoto wanakuwa poyoyo plus
 
Nadhani umetoa maoni bila hata kuangalia video ya mwandishi husika

Alichokifanya mwandishi baada ya kusikia uvumi huo alifunga safari, akawatafuta walalamikaji wakajieleza,

akaenda kwa walalamikiwa wamiliki wa kiwanda wakahojiwa wakajieleza,

akaenda kwa walalamikiwa wa pili ambao ni polisi wanaotuhumiwa kuwatesa na kuwalazimisha kulawitiana, wakahojiwa wakajieleza,

akaenda kwa madaktari waliowapima, wakahojiwa wakasema walichogundua,

Polisi wanasema wamefungua jarada la uchunguzi kuona ukweli wa jambo hilo,

Labda wajuzi wa sheria watusaidie, hapo kosa la mwandishi ni lipi? Nia ovu ya mwandishi iko wapi?

Tukisema mwandishi alilenga kutuhabarisha na kulihabarisha jeshi la polisi kwamba linachafuliwa na hao watuhumiwa mitaani hatutakuwa sahihi?

Hao vijana wako mtaani na wameonekana wakihojiwa na kukiri kuamulishwa kulawitiana na kufanyiwa ukatili mwingine, wao wameshakamatwa ili wakathibitishe walio yasema? Yupi alitakiwa kukamatwa kabla, mwandishi au walalamikaji?

Mimi naona watu wataanza kuhisi mwandishi anataka kunyamanzishwa hivyo watu kujithibitishia kwamba habari ilikuwa kweli kwa sababu ukiangalia ile video ni kama mwandishi anahabarisha tu umma na story ime balance kwasababu wahusika wote wamehojiwa na wameonekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…