Mwanga: Basi kampuni ya Mvungi limepata ajali eneo la Msangeni. Watu 7 wafariki dunia

Watu saba wamefariki dunia papo hapo huku wengine 32 wakijeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Mvungi, walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Kijiji cha Mamba, Kata ya Msangeni, Tarafa ya Ugweno, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Kamanda ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, ambapo amesema ajali hiyo imetokea leo Alhamisi saa moja asubuhi, Aprili 3, 2025 ambapo basi hilo lilikuwa likitoka Ugweno kwenda mkoani Dar es salaam.

Amesema waliofariki katika ajali hiyo ni wanawake watatu akiwemo mtoto mdogo na wanaume wanne.

Ajali hiyo imetokea ikiwa zimepita siku nne tangu itokee ajali nyingine Machi 30,2025 iliyoua watu saba kwa matukio mawili tofauti wilayani Same, ikiwemo iliyoua wanakwaya sita wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mmeni Chome, Dayosisi ya Pare iliyotokea katika milima ya Pare baada ya gari walikuwa wakisafiria kupinduka katika milima hiyo.

Akizungumzia tukio hilo la ajali, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo lilikuwa likijaribu kupishana na gari jingine na ndipo lilipoteleza kwenye tope na kupindika.

ajali mwanga.png

ajalimwanga.png

​
Chanzo Taarifa: mwananchi_official

Kama miaka ya 1993 kuelekea 1994 tulikuwa tukisafiri Milimani huko (kwenda Kusoma Shule ya Shighatini ya Mwalimu Mkuu TK au Marehemu Thomas Kavuye) huku tukiomba Mungu tusipindukie Maporomokoni (hasa katika) hasa katika hiyo Milima hatari ya Ugweno ndiyo iwe katika hii Ajali mbaya iliyotokea Leo?
 
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia baada ya basi kampuni ya Mvungi walilokuwa wakisafiria kupinduka katika milima ya Pare, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kupokea taarifa ya ajali hiyo asubuhi hii, Aprili 3, 2025 na kwamba wapo njiani kuelekea eneo la tukio.

Aidha amesema basi hilo lilikuwa likitokea Ugweno, wilayani humo kuelekea jijini Dar es Salaam.

Hiyo milima ni Noma eeh,Mungu awaponye majeruhi.
 
Mabasi mabovu,yanamaliza raia mwanga!

--
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia baada ya basi kampuni ya Mvungi walilokuwa wakisafiria kupinduka katika milima ya Pare, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kupokea taarifa ya ajali hiyo asubuhi hii, Aprili 3, 2025 na kwamba wapo njiani kuelekea eneo la tukio.

Aidha amesema basi hilo lilikuwa likitokea Ugweno, wilayani humo kuelekea jijini Dar es Salaam.

Umejuaje kuwa lilikuwa bovu?
 
Juzi tena Same
 
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ,hajafika eneo la tukio,bali aliyoyasema ni sisi tumemweleza!
 
Dah! Pole sana Kwa wahanga na wafiwa, Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu
 
Mabasi mabovu,yanamaliza raia mwanga!

--
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia baada ya basi kampuni ya Mvungi walilokuwa wakisafiria kupinduka katika milima ya Pare, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kupokea taarifa ya ajali hiyo asubuhi hii, Aprili 3, 2025 na kwamba wapo njiani kuelekea eneo la tukio.

Aidha amesema basi hilo lilikuwa likitokea Ugweno, wilayani humo kuelekea jijini Dar es Salaam.

UPDATES: WATU SABA WAFARIKI DUNIA
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema watu saba wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la Mvungi na gari dogo kwenye eneo la Ugweno Wilaya Mwanga Mkoa wa Kilimamjaro.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Babu amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa moja asubuni leo Aprili 03, 2025 wakati basi hilo la Mvungi lilipokuwa likitokea Ugweno kuelekea Dar es Salaam.

RC Babu amesema jitihada zinaendelea kunyanyua basi hilo ili kubaini kama kuna miili ama majeruhi.

Poleni sana wafiwa wote. Zamani pale Kinondoni palikuwa na hospitali ya Dr.Mvungi. Alisaidia watu wengi sana yule muungwana.
Ni muda mrefu, kwahiyo sijui nini kinaendelea
 
Poleni wafiwa! Nadhani ni bahati mbaya tu imetokea.
Ajali haina Kinga!
Mungu awape faraja wafiwa,wenye majeruhi pamoja na majeruhi wapone haraka.
 
Back
Top Bottom