Mashangazi bado wanakosea kujifananisha na mabinti wa sasa kwa kigezo cha enzi na zama zao, wanasahau kila zama zina kitabu chake.
Sisi wababa tumekubali matokeo kuwa vijana wetu wa sasa hawawezi na kamwe hawataweza kuishi kama sisi. Ndio maana tukichapiwa wake zetu na marioo, vibenten na boda boda tunajitahidi kusahau tupate usingizi mzuri na tuishi vizuri tu.
Umenikumbusha mkoa wa Tabora kuna chuo kinaitwa uhazili, chuo cha utumishi wa umma pale kuna mabinti hao chuchu saa sita walikuwa wakiwasumbua sana wmashangazi kwa kuwachukulia waume zao, unajua kilichotokea? Mashangazi kwa kutumia influence zao na vyeo vyao walianzisha genge lao la Siri kwa ajili ya kuwadhibiti wababa( waume zao) na mabinti walikuwa wakitoka na hao wanaume.
Mabinti wengi walifanyiwa ukatili wa kijinsia kama kubakwa na kulawitiwa na wahuni waliolipwa pesa na mashangazi.
Kwa kifupi adui wa mwanamke katika ukatili wa kijinsia ni mwanamke mwenyewe.