A
Anonymous
Guest
Barabara ya Mkuyuni, iliyofunguliwa mapema mwaka huu, inaonekana kujengwa chini ya kiwango kinachotarajiwa.
Ikumbukwe kwamba mwezi Aprili kulikuwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha hasara za mali na usumbufu mkubwa wa usafiri. Mimi ni mkazi wa Mwanza, na kwa zaidi ya miaka 20 eneo hilo halikuwahi kushuhudia maji kufikia kiwango cha kujaa kwa daraja kama ilivyotokea mwaka huu.
Cha kushangaza zaidi ni kwamba madhara ya mafuriko yameathiri hata maeneo yaliyo mbali zaidi ya mita 100 kutoka kwenye mradi huo. Aidha, barabara yenyewe haijanyooka na ina miinuko isiyo ya kawaida, licha ya Waziri wa Miundombinu kueleza kuwa imejengwa kwa viwango vinavyokubalika.
Kutokana na hali hiyo, tunaomba TAKUKURU Mwanza pamoja na mamlaka nyingine husika kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ubora wa ujenzi wa mradi huu na kubaini kama thamani halisi ya fedha ilipatikana.