Mwanza City: The Photo Gallery

Tukimaliza quarter ya mwisho wa mwaka na uhakika mapato Ilemela yatavuta 10+ billion
 
Wamiliki wa mabasi wanalalamika udogo wa stendi ya nyamhongolo, imefikia hatua mabasi yakosa sehemu ya kupark, lakini hii stendi tulidanganywa inauwezo wa kupaki mabasi 120 kumbe unawezo wa mabasi 80 tu.
Mbona ni mapema sana
 
Nimefika Mwanza na kuzurula kwa wiki 2 Kuna madhaifu makubwa sana kadhaa nimeyaona.

1- Kwanza Kuna uhaba mkubwa sana wa mtandao wa Rami wa barabara za mitaa. Hii kitu imesababisha Jiji limekuwa disorganized mnooo.

Na ardhi ya Mwanza ilivyo, ni kichanga, bila Rami mvua inanyesha inachota mchanga na kuacha barabara ni mashimo matupu.

Yaani usafiri tegemezi maeneo ya karibu tu ndani ya Jiji yamebaki ni Bajaj na Bodaboda. Mtu nayekaa Kisesa ana afadhali kiusafiri kuliko mtu wa Kishiri, Mahina, Nyanguruguru, nk.

2- Mwanza Jiji Kuna lundo kubwa la kiwanja/maeneo yaliyoachwa tu ambayo hayajulikani ni ya Nani.

  • Hali hii imepelekea kukua na kukomaa kwa genge zito untouchable la matapeli tena wazee kabisa.
  • Kwasababu hiyo kwa uwoga watu wameamua kukacha maeneo ya karibu na kwenda kujazana mbali kabisa ya mji Kama Usagara, Isangijo, Kitumba Kisesa, Mwahuli, Fela, Nyanshishi nk.

Imagine, katikati ya mji kabisa unakuta Kuna watu wanachunga ng'ombe tena wengi kabisa!!!

3- Ubovu wa routes za daladala. Nadhani hili linatokana na pia na Ubovu wa barabra za mitaa. Yaani daldala Ina route ya Magu-Nyanshishi kweli????!!
Mwanza mji unapanuka zaidi kuliko barabara na route za magari, baadaye daladala zinawekwa kwa kulazimisha tu lakini Hali ni mbaya na Tete sana.

4- Majaruba ya kutengeneza kila Kona. Hayo maeneo ni Bora yangepandwa miti kuboresha mji.

Miradi mikubwa iliyopo bado ni hiyo hiyo, soko la makoroboi, stand ya Nyegezi, Daraja busisi.

Kuna upembuzi tu wa barabara za Busenga, Veta- Nyanguruguru, Kuna nyingine Inapita Isela kwenda Kisesa Ila mpaka Sasa bado ni stori tu.

Huu ni mtazamo wangu kwa uzoefu wangu.
 
Hyo stendi runway ni moja tuu Kwa magar yote kuingia na kutoka , sometime unawaza hv hawa wanao_design huwa wanafkria nn
Hii stendi ni ndogo sana, pia magari yanayoingia na kutoka yanapitia barabara moja hii ni jambo la kuchekesha sana.
 
Haya mkuu tuambie nini kifanyike kupunguza hizo hadha, hayo majaruba ya kutengeneza yapo wapi, na hivyo viwanja vingi katikati ya mji vipo wapi nami nikaviangalie?, kuhusu mtandao wa barabara za lami ili ni ukweli lakini sio kusema barabara hazipiti hilo nakukatalia japo ardhi ya Mwanza ni kichanga kama ulivyosema lakini barabara ata kama haina lami zimejengwa kwa changarawe kuwezesha kupitisha magari kwa muda wote wa mwaka pia zimejengewa mifereji ya pembeni.
 
Hii stendi ni ndogo sana, pia magari yanayoingia na kutoka yanapitia barabara moja hii ni jambo la kuchekesha sana.
Mpak sa hv stend imeonekana haitoshi, ndo mana huwa tunasema humu stend ni sehemu ya kushusha na kupakia abiria , la sivyo kila baada ya miaka 5 unahama unajenga stend mpya mbali na mji..mwisho wa sku stend itafika nyangunge , nawaza sjui Kwa nn bara bara ya nyamhongoro hawakuiunganisha Magari yanayotoka yanayoingia yatumie hyo
 
Kuhususu barabara za busenga, kishiri, na nyamhongolo zipo kwenye miradi ya tactic ni jambo la muda tu.
 
Mkuu magari hayakai sana stendi ni mwendo wa kushusha na kupakia na kuondoka lakini mabasi yanakosa sehemu ya kupaki nenda kajionee mkuu.
 
Haya mkuu tuambie nini kifanyike kupunguza hizo hadha, hayo majaruba ya kutengeneza yapo wapi,
Majaruba Mwanza yamejaa kila Kona, kuanzia Buswelu Busenga,Isela, Nyamhongolo, Kisesa n.k.

Viwanja vilivyo wazi ni vingi sana Buswelu, Nyakato, Kangaye, Nyegezi, Nyamhongolo nk.

In short, ukinunua kiwanja Kuna 98% ukatapeliwa.

Hili nazungumza kwa uzoefu kabisa.
Nambie watu wanaoishi Bukaga Kishiri wanaendaje?

Watu wanaoishi Kitumba Kisesa wanaendaje?

Watu wanaoishi Mwahuli, Bujora Kisesa wanaendaje?

Watu wanaoishi Nyakato National wanaendaje?

Watu wanaokaaa Buswelu, Kuna barabara moja tu baadaye ya hapo ni Bajaj au Bodaboda.

Watu wamejaa mpaka Isela huko wanafikaje?

Malimbe, Luchelele huko?
 
Tumia akili acha ujinga ngoja nikuelimishe hayo unayoona majaruba kama macho yako yanavyoona hizo ni "open space" ni viwanja vya halmashauri kwa mipango miji ya baadae.
Et wakazi wa nationa wanafikaje we kweli pimbi, mtaa wa nationa si upo barabara tu hapo nyerere road ata mitaa ya ndani kama gedeli kuna barabara poa tu sema hazina lami.
Naona una mihamko unayokusumbua buswelu iba mitandao ya lami mikubwa sana kwanza barabara ya kutoka sabasaba, kiseke adi buswelu na nyingine inaanzia kona ya veta adi buswelu, kahama adi ilalila.
Kuna coaster nyingi tu zinazotoka mjini kati kupitia kahama adi isela barabara inapitika vizuri sema ya kuelekea isela haina lami.
Kuhusu wakazi wa bukaga kishiri wanafikaje wanafikaje kwani walipojenga huko walikuwa wanafikaje acha uzwazwa, ngoja nikutoe tongotongo kuna miradi ya lami kishiri na fumagila, kishiri wataweka lami ngumu na fumagila wataweka lami nyepesi inayopitia bukaga.
Unauliza kijinga sana et watu wa bujora kisesa watafika wakati kila week naenda bujora kuna lami imeishia ngomeni lakini haijafika bujora japo barabara inapitika vizuri tu na ina trenchi zipo poa lakini jambo la msingi ni kuweka lami adi bujora.
N.B KWANZA UNATAKIWA KUJIULIZA MWANZA IMETOKA WAPI NA SASA TUNAELEKEA WAPI TUSIPENDE KUPONDA SANA TUWE WATU WA SHUKRANI NA MAMBO YOTE HAYAWEZI KUFANYWA KWA MARA MOJA, SUBIRI MIRADI YA TACTIC ITUVUSHEπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Huna facts wewe JUHA. Unaleta matusi unadhani nitakuacha.

Mbwa Koko.
 
Wakuu tubaki kwenye maada yetu ya msingi, penye mazuri hapakosi mapungufu tujikite kwenye kutoa suluhisho la Nini kifanyike. Matusi, kejeli , vijembe na dharau hapa si pahala pake.πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Wakuu tubaki kwenye maada yetu ya msingi, penye mazuri hapakosi mapungufu tujikite kwenye kutoa suluhisho la Nini kifanyike. Matusi, kejeli , vijembe na dharau hapa si pahala pake.πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
Sawa kabisaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…