Mwanza City: The Photo Gallery

Wakuu tubaki kwenye maada yetu ya msingi, penye mazuri hapakosi mapungufu tujikite kwenye kutoa suluhisho la Nini kifanyike. Matusi, kejeli , vijembe na dharau hapa si pahala pake.πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
Kuna watu ni wapumbavu sana, wao ukizungumza wanakurupuka kuanza mashambulizi. Wandhani sisi wengine hatujui kutukana labda.

Mimi nimefika Mwanza, nimekaa muda kidogo na nilikuwa natafuta kiwanja nimezunguka mnooo kuanzia BUSWELU, NYAMHONGOLO, KISESA YOYE, KISHIRI, mpaka MAHINA.

Nimefika kwa Rafiki yangu anaishi MHANDU na ni konda wa daldala. Nimejionea mwenyewe.

Lakini ukizungumza takataka Fulani inakuja juu utafikiri unaitakia Mwanza mabaya.

Mimi kwetu Butiama, nauli ya Mwana kwetu 10,000/= siwezi kukaa naiombea mabaya Lake zone wakati ndio kwetu.

Lazia tuzungumze HALI HALISI ili maboresho yafanyike.


Kiuhalisia Mwanza watu wanajituma sana lakini MAMLAKA zinawaangusha sana watu.
 
Lile jengo la pale Ghana limefikia floor ya ngapi tujuzane
 
Lile jengo la pale Ghana limefikia floor ya ngapi tujuzane
Hilo eneo nilipita nikiwa kwenye daladala, na unajua Mwanza na vi-hiace vidogo ukikosa seat ndio Basi tena hata nje huoni.

Na sikukumbuka kabisa kwenda hapo directly kufanya survey.
 
Nimeipenda hii ya kuiunganisha Isela na Kisesa, Jambo la msingi sana. Mchakato ufanyike haraka sana.
Kuna PLAN ya kuchonga barabara Inapita hapo ISELA chini ya eneo la BUGANDO inaenda nadhani Masemele mpaka KISESA

In short, hiyo Isela imeshajaa watu lakini barabara iliyopo ni Kama Njia ya ng'ombe.

Na baadaye ya muda Bugando wakishaanza ujenzi wa Chuo Chao tayari Inaungana na Magaka, Kahama na Ilalila. Watu wanaanza kwenda nyuma ya Ilalilia huko wanaita Isanzu.
 
M
Mahitaji ni mengi kuliko kipato, ila watapeleka tu barabara. Mahitaji ya kijamii ni kichocheo kikubwa kwa serikali kutoa huduma. Wanajenga mji wa Mtumba wakati hakuna watu au mahitaji hayo kwa sasa.
 
M

Mahitaji ni mengi kuliko kipato, ila watapeleka tu barabara. Mahitaji ya kijamii ni kichocheo kikubwa kwa serikali kutoa huduma.
Nimekaa Arusha na Kilimanjaro huw Kuna utamaduni mmoja mzuri.

Kwa Arusha, Njia za mitaa mara nyingi huwa wenyeviti wa serikali za mitaa wanakubaliana na wanachi wanachunga kila Kaya lets say Tsh 30,000 halafu wanakodi Lori la mchanga wanamwaga mchanga kwenye Njia yote kila mpita Njia anatakiwa apige koleo kadhaa ndio aende.

Pia, kwa Kilimanjaro ( siyo mjini) Kuna siku za maendeleo kuchonga barabara za mitaa na kuzilima zipitike.

Mbinu Kama hizi zingefanyika Mwanza zingesaidia sana.

Kiuhalisia, ili ufurahie Mwanza labda uwe na usafiri wako. Vinginevyo ugharamike Bajaj au Bodaboda.

Maeneo mengi hayafikiki kwa usafiri wa daladala.
 
Naomba Tujitahidi kucontrol hisia zetu, kuna baadhi ya comment sio nzuri kuzisoma zinaudhi.
Tutumie maneno ya staha bila kutukana na kumuudhi mwingine.
JF wangeweka kipengele cha kumwezesha aliyeanzisha uzi kufuta au kuedit baadhi ya comment ingekuwa vizuri zaidi.
 
Mkuu magari hayakai sana stendi ni mwendo wa kushusha na kupakia na kuondoka lakini mabasi yanakosa sehemu ya kupaki nenda kajionee mkuu.
Kitombile usibishe, huwezi niambia kila baada ya saa moja yanatoka mabasi 120, kama stendi haitoshi ni watu Wamegeuza garage.

London ina stendi moja kubwa, hiyo stendi ina mageti kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria, sidhani hata kama yanafika 100.
Basi linakuja kwenye Gate labda dk 15 kabla ya safari, ukifika muda linaondoka saa nyingine dk 5 tu zinatosha hasa kushusha.
Hakuna basi inakaa zaidi, kwa utaratibu huu stendi ni ndogo ila inahudumia basi nyingi kwa siku kuliko stendi kubwa ya nyamhongolo sisi basi inakaa masaa inazibia zingine.
Basi zinazohudumiwa na stendi ya London tukileta nyamhongolo si tutahitaji kata mzima kwa ajili ya stendi tu.
 
In short, kwa uchunguzi wangu sijaona Kama pale ndani hapatoshi kwa Sasa.

Hakuna watu wengi au mabus mengi kwa kiwango hicho useme hapatoshi.

Ukitoka Dar ghafla ukafika Mwanza utaanza kuona Kama vile Mwanza haina watu. Ukitoka stand ya Magufuli ukatua Nyamhongolo utaona Kama stand ya daladala Mbezi Louis Ina watu wengi kuzidi Nyamhongolo.

Binafsi naona walizozingua pale stand ni kuwa na lango la upande mmoja was kuingia na kutokea mabus.

Mabus pale hayawezi kuwa mengi sana Kwasababu mabus yenyewe pale ni Yale ya Mwanza to Musoma, Sirari, na Buhemba pekee.
 
Inaweza kuwa kweli lakini nasikia mabasi hayakai sana, lakini pia tuliambiwa hii stendi inauwezo wa kupark mabasi 120 kumbe ata 80 hayafiki.
 
Inaweza kuwa kweli lakini nasikia mabasi hayakai sana, lakini pia tuliambiwa hii stendi inauwezo wa kupark mabasi 120 kumbe ata 80 hayafiki.
Hata kama inaweza kupaki mabasi 50 kwa wakati mmoja bado ni stendi kubwa.
Waweke utaratibu kwamba basi likikaa Humo ndani zaidi ya nusu saa linakutana na faini getini uone.
 
Please...lugha nzuri hufanya hoja yako ionekane na mantiki .ukitumia lugha ya matusi unaharibu facts zako ..
 
Hata kama inaweza kupaki mabasi 50 kwa wakati mmoja bado ni stendi kubwa.
Waweke utaratibu kwamba basi likikaa Humo ndani zaidi ya nusu saa linakutana na faini getini uone.
Hii stendi ni kubwa mno kwa vyovyote vile haiwezi kujazwa na mabasi labda kama daladala zinaingia mpaka ndani ya stendi. Kusema Buzuruga na Nyamhongolo zinafanana ukubwa sio kweli, nyamhongolo ni kubwa karibia mara 2 ya Buzuruga. Kama Buruga ilikuwa haijazi mabasi iweje nyamhongolo ijae?
Hizi taarifa za nyamhongolo kujaa zimetoka wapi au kuna mtu mmoja kaamua kuzusha?
Halafu kusema basi likae zaidi ya nusu saa lipigwe faini sio sawa. Hii stendi sio kwamba mabasi yanapita yanakuja kuishia hapo na kuanzia safari hapo.
Kwa mfano gari litoke msoma lishushe ndani ya nusu saa linapata wapi abiria wa kujaza halafu ukumbuke halipo moja tu kuna mabasi mengi ya ruti hiyo
 
Stendi ya nyamhongolo.. haiwezi kujaa kiurahisi hivyo .na kama inajaa waondoe tata zote ziishie kisesa..yabaki magari makubwa ...
Stendi ya kisesa isiwe ya hiace za vijijini tu Bali pia hizo tata ziondolew nyamhongolo.zipelekwe huko
 
Nimefananisha ukubwa kwa maana ya uwanja wa katikati wa parking. Kwasababu wanasema Kuna eneo la parking ya maroli nje ya pale ndani.

Kwa stand ilivyo, pande 4!

Upande wa mbele unaotizama na Rami, Kuna mageti ya kuingia abiria, kwa hapo nje ndio wapiga debe wanakaa na daladala zinashusha hapo. Pia Kuna vyumba vya wakata tiketi kabla ya kuingia ndani.

Upande wa nyuma Kuna maduka yanayotazama ndani ya uwanja wa parking wa mabus.

Pembeni, Kuna eneo la mabus kutokea kwenda Musoma na upande wa pili kutokea abiria wa miguu.

Pale ndani siyo pakubwa, ukisimamam unaweza kuona na kuhesabu karibu kila mtu.

Na pia pale ndani hakuna mabus makubwa pekee Kuna mpaka Coaster zinazoenda kama Buhemba.
 
Wamiliki wa mabasi wanalalamika udogo wa stendi ya nyamhongolo, imefikia hatua mabasi yakosa sehemu ya kupark, lakini hii stendi tulidanganywa inauwezo wa kupaki mabasi 120 kumbe unawezo wa mabasi 80 tu.
Stendi Ina capacity ya mabas 120 ,,,kinachowavuruga ni hizo tata za kwenda simiyu ,mugumu,bunda ,kisorya,nyambiti,musoma na kiabakari ...wazipeleke kwenye stendi ya kisesa...ni njia nyepesi isiyo na gharama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…