Mwanza: Daladala kugoma Februari 16, wanadai bajaji zinakwapua abiria wao na kuwamaliza

Mwanza: Daladala kugoma Februari 16, wanadai bajaji zinakwapua abiria wao na kuwamaliza

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
mwanza1.jpg

Wamiliki na madereva wa daladala jijini Mwanza wamesema watasitisha kutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa jiji hilo kufuatia uwepo wa bajaji mjini zinazobeba abiria katika vituo vya daladala na kupelekea wao kushindwa kufanya kazi.

Hayo yamebainishwa kwenye kikao maalum kilichowakutanisha madereva wa daladala, pikipiki na bajaji pamoja na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kikao ambacho kimelenga kusikiliza changamoto walizonazo madereva na kuzitafutia ufumbuzi ambapo madereva wa daladaa wamesema uwepo wa bajaji mjini pamoja na faini za makosa ya barabrani umepelekea wao kufilisika.

Zakayo Mashamba ni dereva bajaji naye akazungumza kuhusu malalamiko yaliyotolewa na wamiliki na madereva wa daladala.

"Wanaoendesha hiache na costa nashukuru leo wamekuwa wawazi tulikuwa tunaona wanazirusha bajaji tulikuwa hatujui kumbe kuna namna, nashukuru leo tumejua, wote sisi ni Watanzania mipaka haiongezeki lakini watu wanaongezeka sasa sisi watu wa bajaji tukale wapi?," amehoji Mashamba.

Wakijibu malalamiko ya wamiliki na madereva wa daladala Mkurugnezi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Aron Kisaka, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Habibu Suluo, wamesema kama madereva wa bajaji wanapakia abiria kwenye vituo vya daladala wanafanya makosa.

Chanzo: EATV
 
Sasa daladala zikigoma kupakia si ndio itakuwa sherehe ya bajaji kupakia kwa raha au wakati wamegoma watazizuia bajaji kupakia?
 
[emoji28][emoji28]naona bajaji siku izi zina taka kuchukua utawala kwa kasi kama kule moshi
Huku ni kukosa ubunifu kwa maafisa wetu wa mipango miji, yaani unaona sawa kuwa na Bajaji 100,000 zenye uwezo wa kubeba watu 300,000 badala ya kuwa na Coaster au Hicher 10,000 zenye uwezo wa kubeba 40,000 mpaka 50,000. Matokeo yake ni msongamano usio wa lazima barabarani na ajali za kujitakia.
 
Sasa wakigoma ndiyo Bajaji zitashindwa kuwachukua wateja wa daladala?
 
Hadi wanafikia hatua huyo maana yake mkuu wa mkoa ameshindwa kulisimamia na kuweka utaratibu mzuri kwa kushirikiana na mkurugenzi wa jiji la Mwanza, that's why migogoro kama hii inashindwa kupata ufumbuzi.
Hapa nafikiri Mkuu wa mkoa ajikatae.
Mkurugenzi wa jiji hatoshi.
 
Back
Top Bottom