Mwanza: Daladala kugoma Februari 16, wanadai bajaji zinakwapua abiria wao na kuwamaliza

Wivu tu na wao wakati abiria wapo wa kutosha mpaka wanasimama kwenye hizo daladala
 
waache uzuzu biashara ushindani wapambane. Sasa wanamgomea nani, je hizo bajaji wakirasimishiwa hiyo biashara hayo magari yao watayafanyia nini. Ningekuwa serikali atakayetoa gari lake barabarani atajua pakuipeleka maana haitarudi barabarani.

IIiwahi kutokea hii ya kufutiwa leseni mwaka 2003 kule kwa akina yakhee wasemaje atii.
 
Hivi hawa dala dala wanafikiri uamzi wao huo utakuwa ni mwarobaini? Wapambane na hali zao hats hao bajaj wanauhitaji ule ule kama wao hivyo kila mmjoja atumie fulsa anayoipata.
 
Na waachwe tu kutoa Huduma, huwezi nishawishi nipande matatu kulingana na uharaka nilionao, na usafiri wa haraka na bei nafuu nauona
 
Sasa daladala zikigoma kupakia si ndio itakuwa sherehe ya bajaji kupakia kwa raha au wakati wamegoma watazizuia bajaji kupakia?
yaani abiria wa jiji la mwanza wahudumiwe na bajaji una chekesha kweli!!halafu huo umbali unaosafiri kwa daladala kwa nauli ya 500,ndio hiyo hiyo utalipia kwa bajaji?!!
 
Biashara huria unakuta gari inapakia massa kibao halafu wanalugha chafu
 
dala dala mlitutesa sana mala mkatize luti matusi kwa makonda wizi nk bajaji kwanza wanaenda na muda hacheni kuogopa ushindani hakuna kazi ya pekeyoko
 
Kule Unguja wakati zinaingia bodaboda na bajaji walipiga majungu sana, mara vibaka, mara wanabeba ovyo wake za watu, mara hawana leseni, mara mara kibaoo.

Kuna binadamu walidhani mpaka mwisho wa dunia ni mwendo wa Vespa, leo kila sehemu, mtu ana namba ya bodaboda wake na mpaka mheshimiwa Dr. Mwinyi anaalikwa kwemda kugawa bodaboda za mikopo.
 
hao wenye vipanya mwanza sio wafanya biashari ya usafirishaji wa abiriya sababu wanaogopa ushindani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…