Mwanza: Familia ya kada CCM aliyetekwa yamuangukia Rais Samia

Mwanza: Familia ya kada CCM aliyetekwa yamuangukia Rais Samia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Familia ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chonchorio maarufu kama ‘Chox’, imemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala la kutoweka kwa mpendwa wao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Machi, Msemaji wa Familia ya Chonchorio, Lucy Mdimi amesema pamoja na mpendwa wao kutoweka siku saba zilizopita, bado haijapata mwanga wa alipo ndugu yao.

Lucy ameiomba Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati ili apatikane kwa kile ambacho alidai alikuwa tegemeo kwa familia huku hofu ikizidi kuongezeka kwa watoto na mke wake.

Amesema Chonchorio ni mtoto pekee wa kiume kwa wazazi wake hivyo, ni tegemeo kwa wazazi wake kuanzisha kiuchumi na kuhudumia familia.

Jana Ijumaa, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza lilitoa taarifa kuhusu mwenendo wa sakata la kada huyo wa CCM na kusema kuwa hadi sasa halijui alipo Daniel Chonchorio maarufu kama ‘Chox’.

Taarifa ya kitofahamika alipo Chonchorio ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa, alipozungumza na waandishi wa habari mkoani humo.


Pia soma:
~
Kada wa CCM aliyepotea Chonchorio inadaiwa alionekana hayupo sawa siku moja kabla ya kupotea, Serikali isaidie apatikane

~ Polisi Mwanza yatangaza kuanza uchunguzi wa tukio la kutoweka kwa Daniel Nyamhanga, Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM
 
Mkiwamaliza wa nje mtakulana wenyewe.haya sasa zamu yenu mlane sawasawa.WATEKAJI WANAFAHAMIKA MPAKA KWA MAJINA NI IDARA YA POLICCM NA WATU WA USALAMA WAKISAIDIANA NA GREEN GUARD YA CCM LAKINI GOVT YA MAMAYETU KIMYA.
 
Mkiwamaliza wa nje mtakulana wenyewe.haya sasa zamu yenu mlane sawasawa.WATEKAJI WANAFAHAMIKA MPAKA KWA MAJINA NI IDARA YA POLICCM NA WATU WA USALAMA WAKISAIDIANA NA GREEN GUARD YA CCM LAKINI GOVT YA MAMAYETU KIMYA.
Duh 🙄 !
 
Kwani CCM nao wanaotekwa????!!!! Kumbe du Sasa tutaimba nyimbo Moja ya wasiojulikana wote,hivi kina soka ,Ben saanane hawakuwa na familia nao??? Kazi iendelee
 
Unatekwa alafu watu wa chama chako wanaogopa hata kukupost mtandaoni. Watu unowaona ni wapinzani kwako ndiyo wanakutafuta. Watu wanaishi kwa mashaka kinoma.

Niliona mke wake akilalamikia watangazaji kugoma kumfanyia interview na kuweka habari za kupotea mshikaji. Sasa hapo waza huyu jamaa ni mbogamboga mwenzao, je sisi wengine itakuwaje
 
Kiongozi wake aliwahi kutuambia kifo nikitu cha kawaida,msipanic!!
 
Back
Top Bottom