Mkuu mnapofanya ulinganishaji wa Kisumu port na Mwanza port sioni uwiano sahihi.
Technical tukilinganisha kwa kuangalia hivi vigezo utaona tofauti kubwa sana
1.Volume of cargo and passenger handled
Mwanza port inahudumia kiasi kikubwa cha meli na mizigo tani nyingi kuzidi Kisumu
2. Port facilities
Mwanza port kuna Tug ship kwa ajili ya msaada wa kuvuta au kusukuma meli iwapo bandarini, kuna crane na winch za kukodi, maji,umeme.
Kisumu port kuna huduma za maji,umeme hakuna winch wala crane pia tug boat na kuna magugu ukienda na meli haina nguvu utapata tabu magugu yakikwama.
3. Implentation of Security
Mwanza port inatekeleza International Ship and Port Facility Security (ISPS Code) kwa level one nikimaanisha kuingia utakaguliwa, utapewa kitambulisho, CCTV na mawasiliano ya radio. Ila kisumu pale security ipo kawaida Sana mgeni akiingia hapewi hata kitambulisho kujua ni visitors au workers.
4. Safety
Mwanza kiwango cha safety ni kikubwa kwa mizigo, wafanyakazi na wabeba mzigo.
Kisumu port pembezoni kuna kichaka cha magugu na kuna viboko huwa wanatoka ziwani, walinzi wanakupa tahadhari usiku usitembee.
Mnapolinganisha Kisumu labda mchague Mwanza South Port au Mwanza Northern Port.