chuki
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 2,715
- 534
Katika hali ya kushangaza Zury Nanji maarufu kama Mwanza Huduma Mfanyabiashara wa Jijini Mwanza ameonekana Bunda Mjini akigawa pesa hadharani.
Huku akiwa na mabaunsa, wapambe na wanakwaya wakimsindikiza Mwanza Huduma amepita Vijiwe vya Kahawa na Maegesho ya Magari na kugawa kati ya shilingi Elfu 50 na laki moja kwa watu hadharani, Pia amepita kwa baadhi ya Mabalozi wa nyumba kumi na kumwaga laki mbili na laki tatu.
Akionekana kujiamini amekusanya baadhi ya wazee katika nyumba moja ya Balozi Semeni Kasuku na kutoa Laki NNE.
Wapambe wa karibu nae wamekabidhiwa shilingi Milioni Moja na kuanza kugawa Elfu kumi Au Elfu kumi na tano kwa Vijana wa Bodaboda na Wanakwaya maalum kwaajili ya kumpamba 'mgombea' huyo.
Kabla tukio hilo la kujitokeza hadharani, Baadhi ya Viongozi akiwemo Mwenezi wa CCM Wilaya Ndugu Bonavencha Makanga akiwa na wasaidizi wake walipita kwa Makatibu wa Kata na kuwapatia posho (rushwa) na baadhi ya Wenyeviti kama sehemu ya salam za Mhindi huyo ambae ameanza kampeni mapema kabla ya muda.
Leo walipoulizwa kwanini wanafanya mambo hayo hadharani bila kuogopa Mpambe wa karibu ajulikanae kama Masalu na Mwingine Selemani Nasoro walisema wamepata kibali kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya hivyo hawatishwi na mtu.
Hali hii isipodhibitiwa Bunda Mjini wagombea watatoana Taya maana Rushwa kwa viongozi wengi inatisha kama Corona.