Mwanza, jiji linaloongoza kuwa na mbuzi watembea bure

Mwanza, jiji linaloongoza kuwa na mbuzi watembea bure

Dar nako maeneo ya Magomeni mbuzi wasio kua na mwenyewe walikua wengi Sana kabla ya wachaga hawajawa wengi Dar. Sasa hivi hata mbwa wanaozurura mitaani shida Sana kuwaona.
Mbwa utawakuta kuanzia kibaha huko na kwenyewe wako mbioni kutoweka.
Wachaga tuna husika vip na upotevu wa mbuzi mkuu?
 
Mbuzi wazururaji nahisi kila mkoa hapa Tz wapo, halafu misosi yao sio majani jombaa, Moshi niliwaona wanakula hadi samaki za kukaanga yani umeweka biashara yako yako ya vitafunwa wakipita hao usipokuwepo andika maumivu.
 
Mwanza Bwana ni Jiji linalokua kwa kasi sana, hilo linatokana na watu kuongezeka na Serikali imeweka miradi mingi ya kimkakati katika jiji hilo, lakini cha ajabu ni kwamba Mwanza ni mji unaoongoza kwa kuwa na mbuzi (wanyama) ambao hawana mwenyewe.

Mara nyingi nimekuwa nikishuhudia mbuzi wakikatiza barabara ya Nyerere kwenda Posta, kinachonishangaza ni kwamba hao mbuzi huwa hawagongwi wala nini, sasa majuzi nimeona Kondoo kabisa!

View attachment 2565551
Hao ni mbuzi wa kisukuma aka mbuzi watu.
 
Back
Top Bottom