KERO Mwanza kuna shida kubwa sana ya maji, na MWAUWASA hawafanyi kitu chochote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mwanza tuna shida kubwa ya maji ambayo imekuwa ikidumu kwa miaka mingi, lakini haiongelewi kabisa. Kwa mfano, maeneo ya Kirumba, maji hutoka mara moja tu kwa wiki, na mara nyingi hutoka usiku wa manane.

Mbaya zaidi, bili za maji zinakuwa kubwa kwa sababu tunalazimika kuacha mabomba wazi kila siku ili angalau tukute hata ndoo moja imejaa. Wakati mwingine tunasahaulika kabisa hadi pale tunapopiga kelele kwa MWAUWASA.

Cha kusikitisha ni kwamba ukiwapigia simu mara ya kwanza, wanapokea na kukuahidi kushughulikia tatizo. Siku ikiisha ukipiga tena, unasikia ujumbe unaosema "your call has been restricted", na hali hiyo huendelea hadi mwezi unaisha.

Jamani, tunateseka sana. Tumeshatuma malalamiko hata wizarani, lakini hakuna majibu. Miaka nenda miaka rudi tunaishi kama tuko jangwani, ilhali Kirumba ipo umbali wa takribani kilomita mbili tu kutoka katikati ya Jiji la Mwanza.
 
Hivi hii issue ni serious kiasi hiki? Kaja Waziri Jumaa Amidu Aweso na bado shida imeshindwa kusolvika?

Source ipo hapo ziwa lina ma millions of cubic meters bado kweli? MWAUWASA na bodi nzima mnazingua bwana.
 
Mwanza inahitaji Ujenzi wa Chanzo kikubwa sana cha Maji kuliko vilivyopo

Chanzo cha Capripoint cha Miaka mingi ns Hiki kipya cha Butimba bado hali ni ngumu

Watu wanaongezeka sana ila vyanzo vilivyopp haviaccomodate ba uongezeko la Watu

Maendi ya Pembezoni kidogo kama Buhongwa, Kisesa, Buswelu aiseeh maji yanaweza toka mara moja kwa wiki mbili
 
Mamlaka ya Maji last time nilikuja wako na ofisi ndogo nasikia sahivi wana majengo mapya ya kishua.

Kwahiyo pesa za kujenga ofisi wanazo, ila intakes za maji hapana.
 
Wana Ofisi kali sana kule mitaa ya Isamilo
 
Hivi hii issue ni serious kiasi hiki? Kaja Waziri Jumaa Amidu Aweso na bado shida imeshindwa kusolvika?

Source ipo hapo ziwa lina ma millions of cubic meters bado kweli? MWAUWASA na bodi nzima mnazingua bwana.
Hali ni Tete mkuu
 
Hilo Ziwa mnafaidika nalo vipi au ndio swimming pool ya Mamba?

Hii nchi. Ninyamaze tu
 
Mwanza tuna shida kubwa ya maji ambayo imekuwa ikidumu kwa miaka mingi, lakini haiongelewi kabisa. Kwa mfano, maeneo ya Kirumba, maji hutoka mara moja tu kwa wiki, na mara nyingi hutoka usiku wa manane.

Mbaya zaidi, bili za maji zinakuwa kubwa kwa sababu tunalazimika kuacha mabomba wazi kila siku ili angalau tukute hata ndoo moja imejaa. Wakati mwingine tunasahaulika kabisa hadi pale tunapopiga kelele kwa MWAUWASA.

Cha kusikitisha ni kwamba ukiwapigia simu mara ya kwanza, wanapokea na kukuahidi kushughulikia tatizo. Siku ikiisha ukipiga tena, unasikia ujumbe unaosema "your call has been restricted", na hali hiyo huendelea hadi mwezi unaisha.

Jamani, tunateseka sana. Tumeshatuma malalamiko hata wizarani, lakini hakuna majibu. Miaka nenda miaka rudi tunaishi kama tuko jangwani, ilhali Kirumba ipo umbali wa takribani kilomita mbili tu kutoka katikati ya Jiji la Mwanza.
Swala la maji ni la nchi nzima. Hii style ya kutoa maji usiku wa manane nayo iko kila sehemu na sijui kwanini wanafanyaga hivyo. Msipoyaotea ndo umetoka hiyo!
 
Back
Top Bottom