Mwanza: Makonda awataka wakandarasi na wazabuni kukamilisha ujenzi wa vivuko kabla ya mwisho wa 2026

Mwanza: Makonda awataka wakandarasi na wazabuni kukamilisha ujenzi wa vivuko kabla ya mwisho wa 2026

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda amewataka Wataalamu, Wakandarasi na Wazabuni wanaohusika na ujenzi wa vivuko Mkoani Mwanza kuhakikisha kazi zote zinakamilika na kukabidhiwa kabla ya mwisho wa mwaka 2026.

Akiwa katika ziara yake mkoani Mwanza, Makonda amesisitiza kuwa vivuko vinavyojengwa, ikiwemo MV Bukondo na MV Ukerewe, vinapaswa kukamilika bila visingizio ili Wananchi waanze kupata huduma za usafiri wa majini.

“Kama mwezi huu utaisha hajaja Mtu kuzindua Mheshimiwa Mwenyekiti na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa chukua kivuko peleka kwa Wananchi,” amesema Makonda.

Ameonya dhidi ya tabia ya kukamilisha miradi lakini kuiacha bila kuanza kutoa huduma kwa sababu ya kusubiri uzinduzi rasmi.

“Serikali yetu haiwezi kutoa pesa alafu Mkandarasi au Mzabuni akamaliza kazi alafu kivuko kinabaki kimesubiri kuzinduliwa,” amesema
 
Back
Top Bottom