Mwanza: Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, John Wegesa Heche achukua fomu ya kugombea Umakamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa'

Haka kanafiki kanadai kwamba Kibaraka Lisu asiichwe mpopokaji eti ni kutukana viongozi ila kanaona ni sawa kabisa Kwa Lisu kumtukana na kumdhalilisha Mbowe.

Sio mara Moja Mbowe amelalamika.

Mbowe Usikubari kuacha Chama Kwa wahuni
 
Heche ni muadilifu. LISSU na HECHE 2025 itakuwa ni 🔥 ✌️✌️✌️
 
Sikuzote tutasimama na lisu
 
Heche kama alivyo Lissu ni mtu mwenye kuichukia RUSHWA.
 
“Nimekaa kimya muda mrefu, nimetafakari muda mrefu, kwanini Watu wanaiunga mkono CHADEMA? kwanini leo kuna Watu wamepoteza maisha kwa ajili ya CHADEMA?, kila nikitoka nyumbani kwangu nje kuna kaburi la Mdogo wangu anaitwa Suguta aliuawa kwenye mapambano ya Chama hiki, sisi tuna alama ipo nyumbani pale, Watu wanatuunga mkono sio kwasababu ya rangi ya nguo tunazovaa ni kwasababu wanaamini tupo kwenye Taifa lililojaliwa rasilimali nyingi sana lakini Watu wetu ni masikini sana”

“Tuna rasilimali za kutosha, ardhi kubwa, mvua za kutosha lakini Watu wetu wanakufa Hospitali kwa magonjwa, Vijana wetu wanamaliza Vyuo hawana matumaini wanafanya betting na wengine wanajigeuza kuwa vibaka, hatuna chakula cha kutosha mpaka leo tunaagiza nje ya Nchi chakula kwasababu walio madarakani kwa miaka 60 wameshindwa kugeuza neema aliyotupa Mungu iwe baraka kwa ajili ya Nchi yetu”

“Haya mambo ndio waliyaona Waasisi wa Chama chetu wakasema tutaunda Chama ambacho kitaleta Viongozi Waadilifu na wenye msimamo ambao watapigania Mamlaka ya Nchi, wakipata Mamlaka ya Nchi wasigeuze kuwa mali yao bali wapiganie maslahi ya Wananchi”

“Leo tuna Watu wachache CHADEMA ambao wamepotoka ambao wanashindwa kujua dhima ya kuanzisha Chama hiki ni nini?, wanataka kufanya malengo ya Chama chetu kuwa malengo binafsi, sisi tunasema hatutokubali, hiki ni Chama cha Watanzania sio cha Wana CHADEMA ndio maana tunachangiwa na Watanzania wote kuendesha Chama hiki”

“Mimi nimekulia kwenye Chama hiki, sijawahi kuwa na Chama chochote zaidi ya hiki, nimewahi kuwa Diwani , Mwenyekiti wa Vijana Taifa, Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, nimekuwa Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu kwa muda mrefu nakijua Chama hiki kwa muda mrefu”

“Mimi namuheshimu Freeman Mbowe na nampenda na nataka niseme mbele yenu kuwa Mbowe kwangu ni Baba wa siasa ambaye amenijenga na siwezi kusema jambo baya kuhusu Mbowe kuna mengi nasikia Watu wanazungumza lakini siwezi kusema, siwezi kutoka hadharani na kusema vibaya kuhusu Mbowe na leo nasema Mwenyekiti Mbowe kwa heshima tutakwenda kwenye Uchaguzi, tutakushinda, nitamuunga mkono Lissu na ninamuunga mkono na nimeamua kuchukua fomu baada ya Wananchi wengi kuongea na mimi kugombea Umakamu Mwenyekiti”
 
CHADEMA Wala rushwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…