Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 ahukumiwa adhabu ya kifo kwa kuwaua watu wawili kwa kukusudia

Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 ahukumiwa adhabu ya kifo kwa kuwaua watu wawili kwa kukusudia

Asante waliopitia magereza wamekuelewa hapa..anakaa jela Kama mwaka mmoja iv afu anakata rufaa..amini kwamba anatoka kiulaini
Wanasema kama kuna watu wenye imani kubwa sana ya kutoka jela basi ni wale waliohukimiwa vifungo vya maisha na wale wa condemn(waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa).

Kosa dogo tu kwenye mwenendo wa ushahidi linawafanya waachiliwe huru kwenye rufaa
 
Nimetamani usimulie zaidi mkuu.

Pa1 na mauhunihuni yangu, kulivyo na kusanyiko la watu eneo la mahakama na vurugu zote zile, mtu anawezaje kuunga mb bila ya kushitukiwa na kadamnasi?

Chaji anaipata na anaunga mb bila wasiwasi duh, emb eleza zaidi mkuu ninufaike.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuwa hivi, mama anavaa kama vile wanavyovaa wakina mama wa nchi za falme za kiaarabu. Wakishatoa hiyo "haramu" kwa mlinzi, kuna chumba ambacho wanakaa mahabusu, basi mama anaruhusiwa kumlisha baba chakula, anajifanya kujibebisha, anashusha zile nguo zake pana kwa hiyo sio rahisi kuonekana sana,...
 
Ilikuwa hivi, mama anavaa kama vile wanavyovaa wakina mama wa nchi za falme za kiaarabu. Wakishatoa hiyo "haramu" kwa mlinzi, kuna chumba ambacho wanakaa mahabusu, basi mama anaruhusiwa kumlisha baba chakula, anajifanya kujibebisha, anashusha zile nguo zake pana kwa hiyo sio rahisi kuonekana sana,...
Yaani umwamba na kujiamini hadi jela!
Ila kwa hukumu hii, kiburi kitaisha chenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upumbavu wa watu wa ile kanda, ubabe ambao hauna maana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wengi wa matajiri wa kanda ya ziwa hela wameipatia kwenye njia za magendo haswa uhalifu.

Kwani si hata huyu mbunge mwenye hela zake ng'ombe zetu katuibia sana.
Halafu ni marafiki wakubwa na mapolisi kwahiyo kwa ishu ndogondogo hupati haki labda ishu nzito kama za mauaji.
 
Mahakama Kuu Mwanza imemhukumu adhabu ya kifo mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi J4, Jumanne Mahende (45) baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kuwaua watu wawili kwa kukusudia. Jumanne alikuwa akikabiliwa na Kesi ya mauaji namba 131 ya mwaka 2015

Anadaiwa kuwa Julai 13, mwaka 2015, saa 4 usiku, aliwaua kwa risasi, Ali Mohamed, fundi ujenzi wa Igoma wilayani Nyamagana na Claude Sikalwanda wa Nyasaka, Ilemela, Mwanza.

Kwa mujibu wa RPC Mwanza, Mkumbo alisema Saa 4 usiku Julai 13 mwaka 2015, mkurugenzi wa kampuni ya mabasi J4 Express akiwa anajiandaa kufunga ofisi yake, alikutana na watu wawili Ally Mohamed (35) na Claude Sikalwanda (35), ghafla ukaanza mzozo uliopelekea Luhende kuwapiga risasi na kufariki papo hapo.

Kwa upande wa ushahidi, mke wa Marehemu Ally Mohamed, Donatha Gabriel na Aziza Sikalwanda ambae ni dada wa marehemu Claude Sikalwanda waliiambia Mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 13 mwezi 7 mwaka 2015 siku ya tukio la mauaji lilipotokea marehemu waliwaaga kuwa wanaenda kuonana na bosi wao ambaye ni mtuhumini.

Inspekta Benidict Manyanda ambae ni shahidi namba tatu katika kesi hiyo aliiambia Mahakama kuwa siku ya tukio alifika eneo la tukio ambapo alikuta miili miwili ya marehemu ikiwa chini na baadae kuipelekea hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Pia soma > Mmiliki wa mabasi ya J4 apiga wawili kwa risasi
Basi zake bado zipo barabarani kweli
 
Hapo sheria imechukua mkondo wake lakini bana haya mambo haya si ajabu akaja kukata rufaa na akashinda.
. .Kama uliweza 'kuwekwa' ndani MIAKA SITA' Ukitafutwa Ushahini wakati ameonekana akiwaua jamaa. Hakuna lisilowezekana Mkuu...
 
Huyo jamaa nilijua hiyo kesi itamkalia vibaya sijui alifikiria nini kuua watu wawili harafu Jamhuri ikuangalie tuu kisa una mabasi...
 
Back
Top Bottom