KERO Mwanza: Soko la Mkolani ni chafu upande wa nyuma, linaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya mlipuko

KERO Mwanza: Soko la Mkolani ni chafu upande wa nyuma, linaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya mlipuko

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Soko la Mkolani, Mwanza, upande wa nyuma ni wa kutisha kutokana na hali ya uchafu. Eneo la kutupia taka limejaa kupindukia hadi kufurika, hali inayosababisha harufu kali isiyovumilika.

Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba ofisi za Wilaya ya Nyamagana zipo umbali wa mita chache tu kutoka eneo hilo. Eneo hili hutumiwa na wafanyabiashara jioni, lakini wakati wa mvua taka hufurika na kusambaa hadi kwenye maeneo ya biashara.

Mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha taka zinaondolewa kwa wakati na eneo hilo linakuwa safi na salama kwa matumizi ya umma.
 
Back
Top Bottom