KERO Mwanza: Tuliosoma Course ya Mortuary Attendant hatupewi kazi, wanapewa ambao hawajasomea

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mkazi wa Mwanza, nimesoma Course ya Mortuary Attendant. Course yetu huwa hutolewa kwa Certificate, hadi sasa tumefika wafanyakazi 200 wa fani hiyo lakini cha kushangaza Serikali imejenga majengo ya mortuary Lakini imesahau kuajiri watumishi wake, naomba mtusaidie na sisi tuweze kupata kazi tunateseka Sana πŸ™πŸ˜­πŸ˜­

Naomba mpaze sauti yetu tunaumia sana kuona watu ambao hawajasoma Course ya Mortuary wapo kwenye vitengo, ambao tumesoma tunateseka mtaani 😭😭😭 Naomba mtusaidie jamani miaka inakimbia na siku zinaenda.

Mim nimeamua kuwasilisha Kero hii kwa niyaba ya wote. Asanteni sana namungu awabariki πŸ™πŸ™πŸ™ Mtukumbuke jamani tupo wengi natunaumia.
​
 
Wahusika walishughulikie.
 
huwa mko sawa sawa kichwani kipindi mnaenda kwenda kusomea hio kozi?
 
Mimi nina mpango kufungua mitambo ya kuchomea maiti, sijui kama hizo fani yako inahusika....
Nitafute kam hauna shida ya kuzichoma badala ya kulala nazo...
 
Mimi nina mpango kufungua mitambo ya kuchomea maiti, sijui kama hizo fani yako inahusika....
Nitafute kam hauna shida ya kuzichoma badala ya kulala nazo...
Hili ni wazo bora na zuri sana , ila naona kama imani za kufufuka na kwenda mbinguni zitakukosesha watejaπŸ€”
 
Hili ni wazo bora na zuri sana , ila naona kama imani za kufufuka na kwenda mbinguni zitakukosesha watejaπŸ€”
Duu kama wale wanataka kuweka mwana ndani sijui itskuaje ?πŸ˜‚
 
Poleni sana, hii ndiyo Tanzania na Serikali yake mambo yanaenda kwa kujuana, undugu nk, jiungeni mpaze sauti kwenye mamlaka husika labda inaweza kusaidia
 
Duu kama wale wanataka kuweka mwana ndani sijui itskuaje ?πŸ˜‚
Hizi labda kwa America na ulaya , kwa Africa atachemka vibya , watu wanasubiri kufa na kufufukaπŸ˜€
 
Pambana ujenge ya kwako
Huwezi amini kuna mwanamke niliwahi kutana nae aliwahi nipa hilo wazo la biashara,

Mortuary, masanduku na gari la kubebea.

Nilimkimbia , mwanamke gani anawaza vitu kama hivyo?
 
Polee mkuu kuna wengine wamesomea ufundi majeneza ajira bila bila(just joke) anyway una umri gani? Nikupe mchongo
 
Huwezi amini kuna mwanamke niliwahi kutana nae aliwahi nipa hilo wazo la biashara,

Mortuary, masanduku na gari la kubebea.

Nilimkimbia , mwanamke gani anawaza vitu kama hivyo?
Hii biashara ni nzuri sana , tena wenye nazo ni wachache mno , na mtu kuiga ni ngumu sana.
 
Mtoa mada how old are you nikupe mchongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…