Mwanza wamebaki na milima yenye mawe, Dhahabu, Geita, Kwa jicho la ndani, Kufurahia kuzaliwa mkoa mpya Geita,ni maumivu kwa jiji la Mwanza!

Hizi ishu za mikoa zipo kisiasa sana. Wewe pambania maisha yako.. kuna watu wanaishi huko Wampembe lakini wana hela nyingi kuliko mtu anayeishi upanga Dar.
Daa nimecheka sana unakuja Hadi Wampembe 🤣🤣🤣🤣🤣

Tena Kuna watu ni wawekezaji wa viwanda vya Samaki huko huko Vijijini na maisha yanaenda.

NB:Ishu ya Mikoa ni muhimu Kisiasa na Ile proudness ya home but pia inasaidia kupata favour ambazo sehemu zingine watakosa Kwa sababu ya status.

Iko kama kwenye maisha ya mtaani mwenye hela au Cheo ndio anapewa heshima kubwa so ni za muhimu sana.

Juzi Mwigulu amasema Kuna Mradi wa AU kujenga hospital za Kimataifa, unadhani watajenga Sumbawanga au Tunduru? 😆😆😆😆

Lazima watajenga kwenye Miji yenye hadhi kama Dom,Dar au Arusha ,swali Kwa nini kiwe na huo utofauti? 👇👇
Tanzania inatarajiwa kuwa miongoni mwa nchi tano za Afrika zitakazonufaika na ujenzi wa mradi mkubwa wa Hospitali itakayokuwa na viwango vya dunia vya utoaji huduma za matibabu (African Medical Center of Excellence (AMCE), kupitia mradi unaotekelezwa na African Export-Import Bank (Afreximbank) kwa kushirikiana na Hospitali ya Chuo Kikuu cha King, iliyoko London nchini Uingereza.

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Umahili cha Kimatibabu, Abuja, Bw. Brian Deaver, wakati Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alipoongoza ujumbe wa Tanzania kutembelea ujenzi wa mradi wa aina hiyo, nje kidogo ya mji wa Abuja, nchini Nigeria.
 
Mwanza intern airport ndiyo suluhisho ya Mwanza vinginevyo serikali inachangia kuiua Mwanza km jiji.
Hata wakijenga Uwanja wa Kimataifa,kama watu wa kusafiri Kimataifa haitawasaidia kitu.

Mbeya Kuna huo uwanja ila hakuna chochote Cha maana.

Mwisho uwanja wa ndege Mwanza jnapanuliwa runway na Passenger buildings unadhani ndio italeta pesa?
 
Hujui kitu, Breweries Mwanza unatia Kodi kubwa kuliko hata hiyo migodi yote iliyoko Geita,kanda ya ziwa na shinyanga,so still mapato wanaopata tu hata Kwa breweries Mwanza
 
Hujui kitu, Breweries Mwanza unatia Kodi kubwa kuliko hata hiyo migodi yote iliyoko Geita,kanda ya ziwa na shinyanga,so still mapato wanaopata tu hata Kwa breweries Mwanza
Sikatai kusema kwamba geita ni kijiji kwa mwanza ila kusema breweries inatoa mapato mengi kuliko mgodi hapo hapana.kibaya siku mgodi wa GGM ukafungwa hakuna tena geita.
 
Angekuwepo Ngosha mikoa yote ya Kanda ya Ziwa ingeng’ara !

Mikoa ina kila kitu madini ya dhahabu na Almasi Pamba na kila aina ya mazao ya kilimo lakini wapiiii !
Hamuna kitu chochote cha maana !
Wajanja wa mujini walishafanya yao !

Ngosha akaishia kusema Tumepigwa 😳
Au tumechezewa sana ndugu zanguni 😅🙌

Au nasema uongo ndugu zanguni ???!! 🤠🤦🏽‍♂️
 
Mwanza na mbeya ni moja ya majiji yanayo kua kwa kasi bila nguvu kubwa ya serikali tofaut na dar,dodoma na Arusha inayo pigwa collable na EAC .kwa mawazo yako unazani Mwanza ina tegemea Geita kua apo
Kweli kabisa mwanza na mbeya ni majisababy ji yanayokuwa kwa haraka sana bila kutegemea mbeleko ya sarikali hasa kwa sababu ya jiografia ya hayo majiji
 
Miaka yake aliing'aeisha Kwa lipi? Tatizo mnakuwa wajinha na wavivu wa kufikiria.

Miaka 5 yake Cha maana hapo Mwanza alichofanya ni Sgr na daraja ambalo halikukamilika.

Mradi mwingine ni Ile ULGDP kuwajengea mastendi tuu ,hakuna jipya zaidi ya Hilo.

Bora hata mama ukiacha kukamilisha Miradi ya Mwendazake ila Kuna miradi Mingi sana ya Barabara ameianzisha.
 
Kwanza mikataba mingi ya madini ni ya kinyonyaji tupu
 
Kufurahia kuzaliwa mkoa mpya Geita, Ni mwanza kuondoka kwenye ufalume wake,

Naomba kichwa cha habari kisomeke hivyo,
Kwan Geita ina muda gani toka iwe mkoa? Mwanza itaendelea umeshakua jiji la kibiashara. Sawa na Arusha tu walivyo ondoa soko la madin ya Tanzanite.
 
Hizi ishu za mikoa zipo kisiasa sana. Wewe pambania maisha yako.. kuna watu wanaishi huko Wampembe lakini wana hela nyingi kuliko mtu anayeishi upanga Dar.
Lakini sasa MamaSamia2025 unataka kuupiga teke ukweli uliopo, hata kama ni kisiasa, ni mhimu kujadiriwa na kuwekwa bayana
 
Kwan Geita ina muda gani toka iwe mkoa? Mwanza itaendelea umeshakua jiji la kibiashara. Sawa na Arusha tu walivyo ondoa soko la madin ya Tanzanite.
Usije kuta miaka kadhaa ihayo wafanya biashara waluopo jijini Mwanza wakaanza kulazimika kufuata bidhaa Katoro Geita
 
Kwa maghorofa haya yanayoibuka kama uyoga hapa Rock City, Geita tuipe miaka 700 kuifikia Mwanza.
Mwanza anaichukulia poa sana huyo jamaa! Kwanza Geita inaingia hata mara 10 kwa Mwanza!
Ndo leo aje aseme Geita iizidi Mwanza!
 
Mwanza anaichukulia poa sana huyo jamaa! Kwanza Geita inaingia hata mara 10 kwa Mwanza!
Ndo leo aje aseme Geita iizidi Mwanza!
Mkuu, mimi nimetoa tu angalizo kutokana na ukweli uliopo, Mwanza inaupungufu mkubwa wa maliasili kama ambavyo ilikuwa na wilaya kama Geita
 
Mkuu, mimi nimetoa tu angalizo kutokana na ukweli uliopo, Mwanza inaupungufu mkubwa wa maliasili kama ambavyo ilikuwa na wilaya kama Geita
Hiyo ishatoka levo ya kutegemea kuchimba madini au kilimo tu! Multieconomical hub kwa sasa!
Mazao Mwanza yanakuja kwa uhitaji uliopo!
Hata ukiangalia uwekezaji wa sekta binafsi Mwanza inatia fora sana hata mtaani Constructions ni kubwa sana ambayo huwezi kuiona popote nchini tofauti na Dar labda na Dodoma kwa kuwa wanajenga Makao Makuu!
 
Hilo wazo lilitolewa na fisadi Magufuri ili ajenge Chato kuwa jiji.
 
Uwekezaji wa miradi ya madini ni temporary,kwa sababu ni no renewable resources,hivyo in long run madini yakiisha ardhini hata hiyo geita itachoka Sana,iangalie miji ya madini duniani ambayo yameshaisha migodi yake je bado Ina flourish,kwa mwanza itajengwa na resources zingine mbali na madini ,sababu madini kwanza hayamnufaishi mtu mdogo,yaanaishia kuibiwa ibiwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…