Mwanza: Wanafunzi Mapacha wa Chuo cha Mipango wafariki Dunia kwa kuzama Ziwa Victoria

Mwanza: Wanafunzi Mapacha wa Chuo cha Mipango wafariki Dunia kwa kuzama Ziwa Victoria

Sasa nini kiliwaua akati wanajua kuogelea???
Kuna baadhi ya sehemu humu ziwani au baharini kuna miamba na hyo sehemu inakua na kina kirefu kweli hata kama unajua ukifika hyo sehemu yenye mwamba lazima yataleta mambo siyo
 
إنا لله وإنا إليه راجعون
Poleni sana wafiwa

Bhujiku ng'waka
 
Hehehe
Nimeshuhudia mara tatu tofauti vifo vya maji. Hivyo sipendi kuwa wa nne[emoji1787]

Kuhusu gegedukastic tampeleka bafuni nafungulia bomba la mvua kisha mambo yanaendele[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Miili ya mapacha Kenny na Lenny Makomonde wenye umri wa miaka 24 waliofariki ndani ya ziwa Victoria walipokuwa wanaogelea wameagwa jijini Mwanza na kuelekea Musoma mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Untitled-3_0.jpg

Inadaiwa mnamo tarehe 28 mwezi huu mapacha hao walienda kuogelea kwenye fukwe za mwalo wa Mihama wilayani Ilemela jijini Mwanza ndipo wakakwama kwenye mapango ya miamba yaliyopo ndani ya ziwa Victoria na kupelekea kupoteza Maisha.

“Ndani ya Maji kulikuwa na mapango ya miamba hivyo waliogolea hadi wakachoka na kushindwa kutoka na wote wakaishiwa nguvu na wote wakazama ndani ya mapango hayo na kupuiteza Maisha na sisi tulipofika tuliwatafuta na kuwakuta wamekwama kwenye mapango hayo ndipo tukawatoa” Amesema msaidizi wa kitengo cha uzamiaji jeshi la zimamoto na uokoaji Mwanza Samweli Nyandito

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Mwanza kamila Labani amewataka wakazi wa maeneo hayo kuacha kuogelea katika eneo hilo kutokana kuwa na hatari kufuatia uwepo wa mapango ya miamba ndani ya mwalo huo ambayo ni hatari kwao.

“Natoa rai kwa wananchi wote wa mkoa wa Mwanza wanaopenda kutumia fukwe kuogelea na siyo fukwe tu hata mabwawa maalum ambayo yanatumika kuogelea wasiende kuogelea bila kufuata kanuni za usalama amabzo ni pamoja na kuvaa makoti maalum yanayomsaidia mtu kuweza kuelea yanitwa lifejacket lakini kamwe wasiogelee kama hakuna mtaalamu wa kuwasaidia kama likitokea tatizo"

Pia soma: Mwanza: Wanafunzi Mapacha wa Chuo cha Mipango wafariki Dunia kwa kuzama Ziwa Victoria
 
Acheni imani potofu za kufikirika. Mnasahau ziwani na baharini kuna mawimbi makubwa yanayoweza kutokea ghafla na kumshinda nguvu muogeleaji mnaleta habari za hallucinations za majini. Majini ni hadithi za kufikirika tu km stori za mazimwi, aliens n.k.

Roho za hao Vijana Zipumzike Mahali Pema Peponi. Amina.
Nafikiri katika hili na wewe inabidi ujitafakari kabla ya kumkosoa mwenzako unaamini yafuatayo ambayo ni ya kiimani tu
1. Unaamini binadamu ana roho kama ulivotamka
2. Unaamini hiyo roho inaendelea kuishi baada ya kifo na unaitakia mema iende peponi
3. Unaamini kuna pepo ambako roho itaenda
4. Unaamini kuna Mungu ambaye anatunza hizo roho


Unaamini hayo na hauna uthibitisho(yapo kifikra) kama mwenzako kisha unakosoa jambo kama hilo
 
Mapacha kwenda kuogelea ziwani pamoja, tena ziwa lenyewe Victoria tena ufukwe wenyewe Mihama kitangiri hiyo rasi imefukia watu wa kutosha. Halafu sijui watu wanamuelewaje huyu Mungu, yaani Mungu awatoe mapacha chuoni sijui mtaani awapeleke ziwani akawazamishe wafe ili mapenzi yake yatimizwe muhhh!! Inafikirisha sana juu ya Mungu wa namna hiyo.

Just imagine
 
Back
Top Bottom