Mwanza: Wanafunzi Mapacha wa Chuo cha Mipango wafariki Dunia kwa kuzama Ziwa Victoria

Mwanza: Wanafunzi Mapacha wa Chuo cha Mipango wafariki Dunia kwa kuzama Ziwa Victoria

Pole Sana,kwa kudhani unajua kumbe hujui hata sekunde mbele moja mbele yako Nini kitakupata.
Sasa Kwa kusema hayo maneno ndo unahs kitu gani kitabadrika ? Tumia akili kusurvive achana na myth story...!! Sio akili unaficha kwenye makalio alaf unaanza kupayuka et Mungu kapanga , Mungu hajawah fanya kazi ya kipuuzi kama hyo
 
Sasa Kwa kusema hayo maneno ndo unahs kitu gani kitabadrika ? Tumia akili kusurvive achana na myth story...!! Sio akili unaficha kwenye makalio alaf unaanza kupayuka et Mungu kapanga , Mungu hajawah fanya kazi ya kipuuzi kama hyo
Duuuh.[emoji1787][emoji1787]
 
Sasa Kwa kusema hayo maneno ndo unahs kitu gani kitabadrika ? Tumia akili kusurvive achana na myth story...!! Sio akili unaficha kwenye makalio alaf unaanza kupayuka et Mungu kapanga , Mungu hajawah fanya kazi ya kipuuzi kama hyo
Uandishi wako tu unaonyesha familia ya namna gani umetokea,siwezi kukulaumu wa kulaumiwa ni waliokukuza
 
Mapacha kwenda kuogelea ziwani pamoja, tena ziwa lenyewe Victoria tena ufukwe wenyewe Mihama kitangiri hiyo rasi imefukia watu wa kutosha. Halafu sijui watu wanamuelewaje huyu Mungu, yaani Mungu awatoe mapacha chuoni sijui mtaani awapeleke ziwani akawazamishe wafe ili mapenzi yake yatimizwe muhhh!! Inafikirisha sana juu ya Mungu wa namna hiyo.
 
Uandishi wako tu unaonyesha familia ya namna gani umetokea,siwezi kukulaumu wa kulaumiwa ni waliokukuza
Tukianza kutukanana wazazi hatutafika naweza kukutukana vile vile , mkuu huna daraja lolote la kujisifia kitabia , kidini hata kimaslah Bora tuishie hapa
 
Maziwa yote yanaweza kuwa na matatizo....hutegemeana na kina ,mzunguko wa maji ,pepo zinazovuma ,majira ya nyakati za mwaka ,uwezo duni wa kuogelea ,human fatalities kama misuli kugoma ,cardiac arrest ...na yale mambo yetu yaleeee....wavuvi wenye HEKIMA tunayajua....[emoji1787][emoji1787]
Duuuh mbna inaogopeshaaa sasa
 
Japo pengine watu watakimbilia ushirikina lakini pengine hiki ndicho kilichotokea.

Kwa vile wote ni waogeleaji wazuri pengine walikuwa wameshaogelea kwa muda mrefu. Inawezekana mmoja alipata tatizo la misuli kukaza na akaanza kuzama. Mwenzake alipoona pacha wake anazama akaenda kumwokoa bila kuchukua tahadhari. Kwa sababu ya panic huyu aliyekuwa anazama akamrukia mwokoaji kwa namna ambayo hakuweza kuogelea tena na wote wakaishia kuzama.

Ni hatari sana kumwokoa mtu anayezama maana anakuwa tayari katika panic mode na anaweza akakung'ang'ania hata mikono ambayo ndiyo unaihitaji sana katika kuogelea. Mtu anayezama inabidi umshike kwa mbali tena kwa mkono mmoja tu halafu umvute huku wewe ukiogelea. Ukijichanganya tu ukamsogelea kuna hatari ya wote kufa. Hapo lazima kuna mmoja amekufa akijaribu kuokoa maisha ya mwenzake.

Na hili tatizo la misuli kukaza aisee linashangaza sana maana hata mimi lilishawahi nitokea. Mimi ni mwogeleaji mzuri tu mpaka wa maji yanayotembea. Nimechukua pia darasa la kuogelea kabisa ili kujifunza jinsi ya kubakia juu ya maji bila kutumia nguvu nyingi.

Sasa siku moja zamani sana nilikuwa naogelea katika bwawa kubwa la hoteli moja iitwayo Omni Resorts kule Orlando, Florida. Nilikuwa nimeogelea kwa zaidi ya masaa mawili na kilichokuwa kimenibakiza pale ni kwamba kulikuwa na mishangazi ya uhakika kibao myeusi na mizungu ipo kwenye bikini tu inajibinua. Basi nikajikuta nimefurahia kutazama ile misambwanda ya kufa mtu huku nasukumizia na chicken wings za hapa na pale. Na mingine tukawa tumezoeana zoeana mpaka tunapiga na vistori vya hapa na pale.

Basi bana baada ya kukaa kwenye kijua kwa muda kwenye hivi viti vya kulaza hivi nikajitosa kule kwenye kina kirefu (futi 12). Eeee bana eeeh!

Najaribu kuogelea hivi hakuna kinachojongea. Misuli imekaza mikono na miguu haisogei. Kengele ya tahadhari ikalia kuwa haki ya nani kuna hatari ya ngosha kufia kwenye pool leo. Na mijimama yote hii dah! Aibu iliyoje!

Nikajaribu tena lakini nikakuta hakuna kinachojongea na hapo tayari nshapiga vikombe kadhaa vikubwa tu. Bahati nzuri sana karibu yangu kidogo kulikuwa na familia ya kizungu inaogelea na mtoto mmoja tineja aliniona akamwambia babake "I think he is drowning". Yule baba alimwita mhudumu mmoja aliyekuwa karibu hapo wana haya mafimbo marefu mwisho yana kama kikofia nchani huwa wanayatumia kuondolea uchafu unaoelea kwenye pool akaninyoshea nikadaka lile lifimbo macho yamenitoka hatari nahema balaa. Wakanivuta nikatoka nje.

Kwa vile nilikuwa nimeogelea pale kwa muda mrefu yule mfanyakazi akawa ananiuliza "What happened?" Nikamwambia I just can't move my hands and legs...Oooh muscle issues. It happens sometimes. Mpaka leo huwa nawaza ningekuwa peke yangu siku ile sijui ingekuwaje [emoji15]

Tangu hapo nikisikia mwogeleaji mzuri amezama wala huwa sishangai. Na baadaye niliambiwa kuwa tatizo hilo linaweza kusababishwa na upungufu wa madini ya Magnesium mwilini na au sehemu fulani ya misuli kukosa hewa ya Oksijeni kwa ghafla. Inapaswa kuwa hydrated pia maana ukiwa dehydrated misuli inaweza kukugomea wakati wo wote. Ulaji wa chungwa moja au mawili pamoja na ndizi pia unasaidia kuzuia tatizo hilo. Wacheza soka na michezo mingine pia wanalijua tatizo hili na sijui huwa wanatumia mbinu gani kulizuia.

[emoji3591][emoji3591][emoji3591] Vijana wadogo tu masikini maisha yao yamekatizwa. Wapumzike salama [emoji1545]
Nakushukuru angalau umetoa possibilities ya kuzama with vivid examples.!
 
Wanafunzi wawili Mapacha wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Mipango Kampasi ya Mwanza wamefariki dunia baada ya kuzama katika Ziwa Victoria wakati wakiogelea katika eneo la fukwe za Mihama Kata ya Kitangiri wilayani Ilemela mkoani Mwanza.


=============

Kenny na Lenny Makomonde (24), mapacha na wanafunzi wa Chuo cha Mipango Kampasi ya Mwanza wamefariki dunia kwa kuzama majini walipokuwa wakiogelea ndani ya Ziwa Victoria.

Tukio hilo lililoacha simanzi na vilio miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho, ndugu, jamaa na marafiki limetokea jioni ya Mei 28, 2023 wakati wawili hao walipokuwa wakiogelea kwenye ufukwe wa Mihama Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Miili ya mapacha hao wanaosemekana kuwa na ujuzi na uzoefu wa kuogelea tayari imepatikana na kuopolewa kutoka majini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakishirikiana na wananchi.

Mkuu wa Jeshi la Zima Moto Wilaya ya Ilemela, Insekta Deusdedith Rutta amesema taarifa za mapacha hao waliokuwa wanasoma kozi ya Mipango na Maendeleo kuzama maji ziliifikia Jeshi hilo Saa 1:00 usiku jana Mei 28, 2023.

‘’Juhudi za uokoaji zilishindikana kutokana na kiwazo cha giza,’’ amesema Inspekta Rutta

Amesema askari wa Zimamoto na Uokoaji walirejea eneo la tukio leo alfajiri kuendelea na uokoaji na kufanikiwa kuopoa miili ya mapacha hao Saa 5:00 asubuhi.

Baba mzazi wa mapacha hao, Makomonde Deus amesima vifo vya watoto wake ni pigo na vimeacha simanzi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa sababu vimetokea ghafla.

"Hatuna la kufanya kwa sababu tunaamini ni mpango wa Mungu. Watoto wangu walikuwa wazefu wa kuogelea na mara kwa mara wanaogelea kila wanapopata nafasi. Kilichotokea ni mipango ya Mungu,’’ amesema Makomonde

Mmoja wa wanafunzi aliyekuwa anasoma darasa moja na mapacha hao aliyejitambulisha kwa jina la Andrew Sengeo amesema vifo vivyo ni pigo na vimeacha simanzi miongoni mwa wanafunzi kutokana jinsi marehemu hao walivyokuwa na ushirikiano na wengine enzi za uhai wao.

Ibada ya kuaga miili ya mapacha hao inaendelea eneo la Chuo cha Mipango kampasi ya Mwanza na juhudi za kupata kauli za viongozi wa chuo hicho kuzungumzia tukio hilo zinaendelea.

MWANANCHI

Sifa za kijinga zitakuwa zimewaponza.
 
Back
Top Bottom